Pata taarifa kuu
SOKA

Rais wa UEFA Michel Platin ataka adhabu ya kadi katika soka iondolewe

Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Michel Platin ametoa wito wa kuondoa adhabu ya kadi ya njano kwenye soka na badala yake wachezaji watakao kiuka sheria za mchezo huo watumikie adhabu ya kosa hilo kwa namna nyingine. 

Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Michel Platin
Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Michel Platin theguardian.com
Matangazo ya kibiashara

Platin amesema kuwa angeweza kubadili mfumo wa kutoa tahadhari na kadi kwa kumtoa mchezaji nje ya mchezo kwa dakika 10 au 15 kutumikia adhabu ya kosa alilolitenda kama inavyofanyika kwenye mchezo wa raga.

Mkuu huyo wa UEFA maeongeza kuwa kwa kufanya hivyo italeta manufaa kwa timu pinzani ya mchezaji huyo katika mechi hiyo badala ya kikwazo cha kadi ambacho hupelekwa mbele dhidi ya timu ya tatu itakayocheza nayo katika kalenda ya soka.

Chini ya mfumo uliopo sasa, mchezaji ambaye anapata kadi nyekundu moja kwa moja au kadi mbili za njano katika mchezo mmoja hutolewa nje ya mchezo mara moja na nafasi yake haijazwi na mtu mwingine.

Lakini mchezaji ambaye atakusanya kadi kadhaa za njano katika mechi mbalimbali anaweza kusimamishwa kucheza mechi zijazo katika mashindano hayo hayo.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.