Pata taarifa kuu
SOKA-ULAYA

Timu ya Bayern Munich yaelekea Moscow huku ikimwacha mshambuliaji wake nyota Mario Mandzukic

Timu ya Beyern Munich inaelekea jijini Moscow nchini Urusi kwa ajili ya mchezo baina ya timu hizo mbili na kwa ajili yamchezo wa ligi ya mabingwa baina yake na CSKA siku ya Jumanne , huku ikimkosa mshambuliaji wake nyota,Mario Mandzukic. 

Kikosi cha timu ya Bayern Munich
Kikosi cha timu ya Bayern Munich wholles.com
Matangazo ya kibiashara

Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Croatia ambaye anasumbuliwa na tatizo kwenye eneo la chini ya goti , anaungana na wachezaji wenzake ambao ni majeruhi, Frank Ribery na Bastian Schweinsteiger ambao kwa pamoja wamebaki nyumbani.

Katika kuweka sawa idadi ya wachezaji, Kocha Pep Guardiola amewaita kwenye timu wachezaji wa akiba Pierre Emile Hojbjerg, MitchellWeiser na Julian Green.

Bayern ambayo kwa sasa wanashikilia ubingwa wa ligi hiyo , tayari wamefuzu katika hatua ya mtoano ikiwa imeshinda michezo yote minne ambayo tayari imecheza huku ikiwa na michezo miwili ya kundi D mkononi.

Lolote litakalo tokea mjini Moscow, Bayern inahitaji sare nyumbani itakapocheza na Mancester City katika mchezo wao wa mwisho utakao chezwa mnamo Disemba 10 ili kujihakikishia inamaliza kwa ushindi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.