Pata taarifa kuu
RAGA

Wachezaji 6 wa raga nchini Australia waadhibiwa kwa kosa la kutumia pombe

Kocha wa timu ya Taifa ya raga nchini Australia Wallabies, Ewan McKenzie, amewafungia wachezaji sita kutoshiriki mechi moja kwa kosa la kunywa pombe katikati ya wiki kabla ya mechi ya mwishoni mwa juma baina yao na Ireland ambapo Australia waliibuka na ushindi. Wachezaji waliofungiwa ni Adam Ashley Cooper, Nick Cummins, Liam Gill, Tatafu Polota-Nau, Benn Robinson na Paddy Ryan.

Chris Hyde
Matangazo ya kibiashara

Wachezaji hao hawatashiriki mechi dhidi ya Scotland mwishoni mwa juma hili, kasoro Ryan pekee ambaye atatumikia adhabu yake kwa kutoshuka dimbani wakati Australia watakapochuana na Wales.

Kocha McKenzie amesema wachezaji hao walifanya kosa la kukaa nje usiku na kutumia kiasi kikubwa cha pombe, suala ambalo ni kinyume na maadili ya Taifa hilo.

Adhabu hiyo imekuja sambamba na onyo kwa wachezaji wengine tisa ambao wametakiwa kujirekebisha baada ya kukiuka maadili ya mchezo huo.

Kocha McKenzie amesema anatambua kuwa adhabu hiyo itasababisha upungufu mkubwa kutokana na kokosa wachezaji mahiri, lakini anaamini huo ni ujumbe mkubwa ili kurekebisha tabia za wachezaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.