Pata taarifa kuu
MPIRA WA MIGUU

Coleman aongeza mkataba kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Wales

Chama cha soka nchini Wales kinaelezwa kuingia mktaba wa miaka mwili zaidi na kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Chris Coleman, hatua inayokuja baada ya miezi kadhaa ya uvumi kuwa huenda angeachana na timu hiyo. 

Chris Coleman, kocha mkuu wa timu ya taifa ya Wales
Chris Coleman, kocha mkuu wa timu ya taifa ya Wales Reuters
Matangazo ya kibiashara

Coleman anatarajiwa kutangaza uamuzi wake wa kusalia kukinoa kiosi cha timu ya taifa ya Wales hii leo kwenye uwanja wa Cardiff ambako anatarajiwa pia kujibu maswali ya waandishi wa habari kuhusiana na kibarua chake.

Kwa mantiki hiyo sasa ni wazi Coleman atahusika moja kwa moja na kukinoa kikosi hicho kuelekea kufuzu kukata tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2016.

Mkataba wa Coleman unatarajiwa kumalizika hapo kesho mara baada ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taufa ya Finland.

Timu ya taifa ya Wales imemaliza kwenye nafasi ya tano kwenye kundi lake la A kwenye kuwania kukata tiketi ya kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia nchini Brazil.

Kuongeza mkataba na timu ya taifa ya Wales kunakuja kufuatia majuma kadhaa ya uvumi kuwa huenda kocha huyo akasitisha mkataba wake na kuchukua nafasi ya ukocha kwenye klabu yake ya zamani ya Crystal Palace.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.