Pata taarifa kuu
RIADHA-JAMAICA

Kamati kuu ya Wada kukutana kujadili suala la wanariadha kukwepa kupima afya kubaini iwapo wanatumia dawa za kusisimua misuli

Mkurugenzi wa zamani wa shirika la kupinga matumizi ya wanamichezo kutumia dawa za kusisimua misuli nchini Jamaica, ameonya kuhusu tabia iliyozuka hivi karibuni kwa wanariadha wa nchini humo kukwepa kupimwa iwapo wanatumia dawa hizo au la. 

Mwanariadha wa Jamaica, Sherone Simpson na Asafa Powell
Mwanariadha wa Jamaica, Sherone Simpson na Asafa Powell Reuters
Matangazo ya kibiashara

Dr Paul Wright ambaye ni mkuu wa kitengo cha upimaji kwenye shirika la Jadca anasema kuwa licha ya hatua zinazotaka kuchukuliwa na Wada bado haoni tatizo hilo kumalizika nchini Jamaica kwakuwa tayari kuna mapungufu kwenye sheria za kuongoza mchezo huo.

Kauli ya Dr Wright inakuja ikiwa imepita wiki moja tu toka ujumbe wa shirika la kimataifa linalopinga matumizi ya dawa za kusisimua misuli mchezoni WADA ufanye ziara yake nchini Jamaica kwa lengo la kufanya tathmini ya namna ya kukabiliana na tatizo hilo.

Nchi ya Jamaica imeingia kwenye kashfa ya wanamichezo wake kukwepa upimwaji wa afya zao kubaini iwapo wametumia dawa hizo au la kufuatia ripoti ya chama cha mchezo wa riadha na kile cha Jadca kudai kuwa kilifanya uchunguzi wa wanamichezo wake mara moja tu katika miezi sita ya mashindano kabla ya mwezi June mwaka huu.

Mkuu wa zamani wa shirika la Jadca nchini humo, Renee Anne Shirley alinukuliwa hivi karibuni akikiri shirika lake kufanya uzembe kwenye kupima wanariadha wake kabla ya kwenda kwenye mashindano na kwamba jambo hilo linaiweka Jamaica kwenye ramani mbaya ya mchezo wa riadha.

Mwezi June mwaka huu, mwanariadha wa mbio za mita 100, Asafa Powell na mwenzake Sherone Simpson walibainika kutumia dawa za kusisimua misuli kabla ya mashindano ya kitaifa mwezi June mwaka huu.

Asafa mwenye kwenye mahojiano yake amekiri kuwa alitumia vidonge lakini hakufahamu kuwa vingeweza kusisimua misuli yake kuelekea mashindano ya riadha ya taifa kuchagua wanariadha watakaoiwakilisha nchi hiyo.

Kamati kuu ya Wada inatarajiwa kujadili ripoti yake iliyokusanya toka nchini Japan kwenye mkutano wake wa mwaka mjini Johannesburg, Afrika Kusini ambapo mkutano huu unatarajiwa kutoa mapendekezo kuhusu hatua za kuchukua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.