Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA UINGEREZA

Beki wa Manchester United Nemanja Vidic aruhusiwa kutoka hospitalini

Nahodha wa timu ya Manchester United ya nchini Uingereza, Nemanja Vidic ameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kupata majeraha wakati wa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Arsenal.

Beki wa kati wa manchester United, Nemanja Vidic akitolewa nje ya uwanja baada ya kuumia
Beki wa kati wa manchester United, Nemanja Vidic akitolewa nje ya uwanja baada ya kuumia Reuters
Matangazo ya kibiashara

Vidic alilazimika kutoendelea na mchezo wa Jumapili dhidi ya mahasimu wao klabu ya Arsenal baada ya kugongana na mlinda mlango wake, Daivid De Gea wakati wakijaribu kuokoa mpira uliokuwa ukielekea langoni mwao.

Mara baada ya kuanguka Vidic aliweza kusimama tena lakini akashindwa kuendelea na mchezo na kukimbizwa hospitali kwa uchunguzi zaidi baada ya kuchukua muda uwanjani wakati madaktari wa timu wakimkagua.

Kwenye taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa klabu hiyo wa www.manutd.com, imesema kuwa Nemanja Vidic ameruhusiwa kutoka hospitali na sasa atakuwa nje ya uwanja kwa angalau wiki moja zaidi na anatarajiwa kurejea tarehe 24 ya mwezi huu wakati timu yake itakapocheza na Cardiff.

Taarifa hiyo imesema kuwa Vidic aliumia sehemu ya taya na sehemu ya kichwa kutokana na kujigonga kwa nguvu na mlinda mlango wake.

Hivi karibuni mlinda mlango wa Tottenham, Hugo Lloris aligongwa sehemu ya kichwa na madaktari wake kumruhusu aendelee na mchezo jambo ambalo lilikosolewa vikali na wataalamu wa soka wakihofia afya yake.

Kwenye mchezo wa Man utd na Arsenal, Man utd ilifanikiwa kuchomoza na ushindi wa 1-0 dhidi ya Arsenal.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.