Pata taarifa kuu
Football-ligi ya mabingwa

Barcelona, Atletico zatinga hatua ya mtoano kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya

Klabu za soka za nchini Uhispania, Barcelona na Atletico Madrid zimefuzu kutinga hatua ya mtoano katika michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani ulaya baada ya mechi zao za nyumbani zilizopigwa siku ya jumatano.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Barcelona wametinga nafasi hiyo baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya AC Milan ya Italia kupitia mechi yao ya kundi H iliyopigwa katika dimba la Camp Nou.

Lionel Messi ambaye amekuwa akilalamikiwa kwa kutopata mabao katika michezo mitatu iliyopita, ndiye aliyeipachikia Barca mabao mawili katika mechi hiyo na jingine lilipachikwa na Cesc Fabregas.

Atletico nao wanafuzu katika hatua hiyo kwa mara ya kwanza toka msimu wa mwaka 2008-2009, nafasi hiyo wamepitia kupitia ushindi dhidi ya Austria Vienna kwa jumla ya magoli 4-0.

Mabao ya Atletico yalipachikwa kimiani na Miranda, Raul Garcia, Filipe Luis na Diego Costa.

Wakati huo huo Arsenal wameibuka na ushindi wa ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Borussia Dortmund waliokuwa wenyeji wa mtanange huo nchini Ujerumani.

Bao la pekee la Arsenal lilipachikwa na Aaron Ramsey katika dakika ya 62 ya mchezo huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.