Pata taarifa kuu
football-Australia

Kipa wa timu ya taifa ya Australia Mark Schwarzer atangaza kuachana na soka la kimataifa

Shirikisho la Soka nchini Australia, limetangaza kwamba mlinda mlango wa timu ya taifa Mark Schwarzer ameamuwa kusitisha kucheza soka la kimataifa akiwa na umri wa miaka 41, hatuwa ambayo ameichukuwa wakati timu yake ya taifa tayari imefuzu kucheza kombe la dunianchini Brazil mwaka 2014.

Mark Schwarzer Golkipa wa Australia
Mark Schwarzer Golkipa wa Australia
Matangazo ya kibiashara

Schwarzer, aliliambia shirikisho la michezo nchini mwake kwamba amesitisha kuichezea timu hiyo, wakati ambapo tayari alikuwa ameorodheshwa katika wachezaji wa timu hiyo wataopambana na Costa Rica katika michuano ya kimataifa ya kirafiki Novemba 19.

Schwarzer, ameitwa mara 109 kuichezea timu yake hususan katika kombe la dunia mwaka 2006 na 2010, lakini pia fainali ya kombe mataifa ya Asia mwaka 2011.

kwa sehemu kubwa kipa huyo wa Australia amecheza soka la kimataifa katika klabu ya  Brandford City iliokatika daraja la pili nchini Uingereza kuanzia mwaka 2006-2007, Middlesbrough (1997-2008), Fulham (2008-2013) na Chelsea ambako ameichezea klabu hiyo mechi 500 katika ligi kuu nchini Uingereza.

Akiwa katika klabu ya Chelsea, msimu huu amecheza mechi mbili katika michuano ya kombe la ligi.

Schwarzer, ambaye wazazi wake ni Wajerumani waliokimbilia nchini Australia katika miaka ya 1960 alianzia kucheza soka nchini Ujerumani katika ligi kuu nchini humo katika vilabu vya Dynamo Dresde et à Kaiserslautern.

kutangaza kusstafu kwa mlinda mlango huyo kunatowa nafasi kwa vijana wengine chipukizi kurithi mikoba hiyo, ambapo majina yanato tajwa ni pamoja na Mitch Langerak, kipa msaidizi wa klabu ya Borussia Dortmund,na Mathew Ryan, kipa wa  FC Bruges daraja la kwanza nchini Ubelgiji.

Hatuwa hiyo ya kuachana na soka ya kimataifa, imewashtuwa wachezaji wenzake wa timu ya taifa lakini pia viongozi wa soka nchini humo.

wakati akiitwa kwa mara ya 109, timu yake iliadhibiwa vikali katika mechi ya kirafiki na Brazili kwa kutandikwa mabao 6 kwa 0 Semptemba 7, huku baadae Octoba 11 timu hiyo ikachapwa na Ufaransa mabao 7 kwa sufuri ambapo mechi hiyo hakuwepo langoni. Tukio ambalo lilisababibisha kocha Holger Osieck kufurushwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.