Pata taarifa kuu
UJERUMANI

Kashfa ya kukwepa kodi kumkabili rais wa Bayern Munich Uli Hoeness

Rais wa klabu ya Bayern Munich Uli Hoeness atakabiliwa na kesi ya madai ya kuficha mamilioni ya Euro kutoka katika mamlaka za kukusanya kodi, kenye akaunti ya benki moja nchini Uswisi mahakama imearifu.

Rais wa klabu ya Bayern Munich Uli Hoeness
Rais wa klabu ya Bayern Munich Uli Hoeness port01.com
Matangazo ya kibiashara

Mahakama kuu ya kanda mjini Munich imeeleza katika taarifa yake kuwa imekubali kusikiliza kesi iliyofikishwa mahakamani hapo na waendesha mashataka wa umma mwezi July na kwamba kesi hiyo itaanza kusikilizwa mnamo Machi 10.

Rais huyo wa Bayern mwenye umri wa miaka 61 anatuhumiwa na waendesha mashtaka mjini Munich kwa kukwepa kodi madai ambayo hayajatolewa ufafanuzi zaidi kutokana na matakwa ya usiri katika kushughulikia madai ya kodi kabla ya kusikilizwa hadharani.

Waendesha mashtaka wamefungua madai hayo dhidi ya kiongozi huyo wa juu wa mabingwa wa Ulaya baada ya uchunguzi wa hali ya juu kufanywa kwa miezi kadhaa na kutikisa idara ya michezo na siasa nchini Ujerumani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.