Pata taarifa kuu
Michezo

Kocha wa timu ya taifa ya Uswisi atajiuluzu baada ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil

Kocha wa timu ya taifa ya Uswisi Mjwrumani Ottmar Hitzefeld ametangaza kwamba ataondoka katika nafsi hiyo punde tu baada ya kombe la dunia la mwaka 2014 nchini Brazil.

Kocha wa timu ya taifa ya Uswisi Ottmar Hitzefeld
Kocha wa timu ya taifa ya Uswisi Ottmar Hitzefeld
Matangazo ya kibiashara

Kocha huyo raia wa Ujerumani anaongoza timu hiyo ya taifa ya Uswisi tangu Julay Mosi mwaka 2008 amekataa kusaini mkataba mwingine na shirikisho la soka nchini humo akieleza kuwa atakuwa na umri wa miaka 65 mwezi Januari na utakuwa ni wakati muafaka wa kusitisha kazi hiyo baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka thalathini.

Katika mkutano mfupi na vyombo vya habari jijini Berne, kocha huyo wa zamani wa vilabu vya Borussia Dortmund na Bayenr Munich, Ottmar Hitzefeld amesema huu ni uamuzi mzito kuuchukuw akatika maisha yake ya soka.

Uamuzi huu umekuja baada ya timu ya taifa ya Uswisi kufaanikiw akukata tiketi ya kuelekea kwenye kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

Kiongozi wa shirikisho la soka nchini Uswisi Peter Gilliéron amesikitishwa na hatuwa hiyo inayokuja baada ya taifa hilo kufaanikiw akufuzi kucheza michuano ya kombe la dunia katika historia yake, lakini kutokana na sababu alizozitowa kocha huyo, kiongozi huyo ameendelea kusema wanaheshimu maamuzi yake.

 

Ottmar Hitzefeld amekuwa akikosolewa baada ya kushindwa kufaakisha timu hiyo kufuzu michuano ya mataifa bingwa baranai Ulaya, lakini kwa sasa amekuwa akionekana kuw amtu maana baada ya timu yake kufanya vizuri ambapo timu hiyo imecheza michezo 14 bila kupoteza.

Mbali na kufaanikiw akufuzu kombe la dunia, imeshinda michezo 7 huku ikigawa michezo 4, lakini pia timu hiyo ilifaanikiwa kuichapa Brasil bao 1 kwa 0 katika michuano ya kirafiki mwezi Agosti iliopita.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.