Pata taarifa kuu
Football

Paris St Germain, Manchester United, Manchester City, Bayern Munich zatamba katika mechi za ligi ya mabingwa barani Ulaya

Klabu ya Manchester United hapo jana imeilaza Bayern Liverkusen kwa mabao 4-2, Wayn Rooney hapoa jana alikuwa kinara wa mchezo baada ya kupachika nyavuni mabao mawili ambapo bao lake la kwanza alilipachika katika dakika ya 22’, na ya 70, huku Vana Parsy naye akiweka nyavumi bao moja katika dakika ya 59. Mchezaji Valancia alifaulu kupachika bao la nne la Manchester United katika dakika ya 79. 

Mshambuliaji wa Manchester United na Timu ya Taifa ya Uingereza, Wyne Rooney
Mshambuliaji wa Manchester United na Timu ya Taifa ya Uingereza, Wyne Rooney Yahoo
Matangazo ya kibiashara

Upande wa Banyern Liverkusen mshambuliaji Rolfes aliweka nyavuni bao lake katika dakika ya  54’ huku Toprak akiweka bao la pili la klabu hiyo katika dakika ya 88’.

Katika mechi nyingine ya hapo jana kalbu ya Real Madrid imeinyeshea mvua ya mabao Galatasaray anayo chezea Didier Drogba mjini Istamboul kwa kuipa mabao 6-1. Mshambuliaji Gareth Bale, Christiano Ronaldo, Karim Benzema na Isco ndio waliokuwa vinara wa mchezo huo.

Manchester City nayo ilikuwa uwanjani jana kumenyana na Victorian Plzen na kuilaza kwa mabao 3-0, maboa ambayo yalipachikwa uwanjani na Dzeko katika dakika ya  48’ Touré 53’ Agüero 58’.

Paris Saint Germain ya Ufaransa nayo imeilaza Olympiakos kwa mabao 4-1, upande wa PSG mabao yaliwekwa nyavuni na Cavani katika dakika ya 19’ na Motta 68’, ambaye aliongeza lingine katika dakika ya 73’ huku Marquinhos ikisindiria msumari katika dakika ya 86’. Upande wa Panatinaikos mchezaji Weiss ndiye ambaye alifunga bao la kufutia machozi katika dakika ya 25’.

Bayern nayo iliifunza kandanda CSKA Moscou kwa kuichapa mabao 3-0 , mabao ambayo yalipachikwa nyavuni na Alaba katika dakika ya 3’ Mandžukic katika dakika ya 41’  na Robben katika dakika ya 68’.

Matokeo mengine ya mechi za jana Juventus ilikwenda sare na FC Copenhagen kwa kufungana bao 1-1, huku Benfica ikiilaza Anderlech mabao 2-0, Shaktar donetsk iliifunga Real Sociedad mabao 2-0

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.