Pata taarifa kuu
OLIMPIKI

Thomas Bach ateuliwa kuwa rais mpya wa kamati ya Olimpiki, achukua nafasi ya Jacques Rogge anayemaliza muda wake

Kamati ya Olimpiki ya dunia hatimaye imepata rais mpya anaechukua nafasi ya Jacques Rogge ambaye hapo jana alimaliza muda wake rasmi wa kuitumikia kamati hiyo.  

Thomas Bach, rais mpya wa kamati ya Olimpiki - IOC
Thomas Bach, rais mpya wa kamati ya Olimpiki - IOC REUTERS/Alexander Hassenstein/Pool
Matangazo ya kibiashara

Wajumbe wa Olimpiki kwa kauli moja walimchaua Thomas Bach raia wa Ujerumani kuwa rais mpya wa kamati ya Olimpiki baada ya Rogge kumaliza muhula wake wa miaka 12 kama rais wa kamati hiyo.

Bach mwenye umri wa miaka 59 anakuwa rais wa tisa wa kamati ya Olimpiki kwenye historia ya miaka 119 toka kuanzishwa kwa kamati ya Olimpiki ya dunia.

Bach alikuwa miongoni mwa wajumbe wengine sita ambao majina yao yalipendekezwa kuwania nafasi hiyo mjini Buenos Aires nchini Argentina kwenye zoezi ambalo lilishuhudia kura zikirejelewa mara mbili.

Mara baada ya uteuzi wake Bach amewapongeza wajumbe wa Olimpiki kwa kuonesha imani yao kwake na kuamua kumpa kura ambazo sasa zinamwezesha kuingia kwenye historia ya kuliongoza shirikisho hilo.

Rais huyo mpya amekiri kukabiliwa na changamoto nyingi mbele yake katika kuhakikisha mashindano yao yanaendelea kifanikiwa kila mara nchi wanachama inapopewa jukumu la kuandaa mashindano.

Nae rais anayemaliza muda wake Jacques Rogge amewapongeza wajumbe wa kumuonesha ushirikiano kwa kipindi chote cha miaka 12 ambayo amelitumikia shirikisho la Olimpiki ambapo amewatakia kila laheri katika kuendeleza shughuli zake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.