Pata taarifa kuu
US OPEN

Serena Williams atwaa taji lake la tano la michuano ya US Open, aingia kwenye vitabu vya historia

Mchezaji Tenesi nambari moja duniani kwa upande wa wanawake Serena Williams amedai kuwa angeshindwa kutwaa taji la US Open kwa mwaka huu ungekuwa ni mwaka wake mbaya zaidi kwenye historia ya mchezo huo.

Serena Williams (kulia) akipongezwa na mwenzake, Victoria Azarenka (kushoto)
Serena Williams (kulia) akipongezwa na mwenzake, Victoria Azarenka (kushoto) Reuters
Matangazo ya kibiashara

Serena ambaye alikuwa akitetea taji lake, ameibuka na ushindi baada ya kumfunga Victoria Azarenka kwa seti mbili moja kwa matokeo ya 7-5, 6-7 na 6-1 kwenye mchezo ambao ulilazimika kuchezwa kwa zaidi ya saa mbili.

hili linakuwa ni taji lake la tano la ubingwa wa michuano ya US Open na pia ni taji lake la pili kubwa kulitwaa ndani ya mwaka huu kufuatia pia ushindi wake wa michuano ya French Open.

Mara baada ya mchezo huo, Serena amesema hakutarajia mchezo mrahisi kutokana na aina ya mchezo ambao Azarenka anacheza na kwamba ushindi wake ulikuwa mgumu zaidi ukilinganisha na michuano ya French Open.

kwa ushindi huo sasa Serena anaingia kwenye vitabu vya historia kwa upande wa wanawake kwa kuwa mwanamke mwingine mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kutwaa taji hili na pia mataji 17 ya mchezo huo.

Serena hakuwa na msimu mzuri kwa mwaka huu baada ya kupoteza pia taji la Australian Open baada ya kutolewa kwenye hatua ya robo fainali na mwanadada Sloane Stephens na kisha kutuowa nje kwenye michuano ya Wimbledon kwa kfungwa kwenye hatua ya nne na Lisick Sabine.

Leo ni fainali kwa upande wa wanaume ambapo Rafael Nadal atakutana na mchezaji nambari moja kwa mchezo huo upande wa wanaume, Novak Djokovic.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.