Pata taarifa kuu
SOKA-JAPAN-BRAZIL

Timu ya Taifa ya Japan imetangaza kutumia Mashindano ya Kombe la Mabara kama sehemu ya maandalizi ya Kombe la Dunia 2014

Timu ya Taifa ya Japan imesema itatumia Mashindano ya Kombe la Mabara kama sehemu yao ya maandalizi kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika mwaka nchini Brazili. Japan imekuwa timu ya kwanza kukata tiketi ya kufuzu kwa ajili ya Mashindano ya Kombe la Dunia baada ya kufanikiwa kupata sare ya kufunagana goli moka kwa moja na wapinzani wao Australia.

Mchezaji wa Japan Keisuke Honda akifunga mkwaju wa penalti katika mchezo dhidi Australia na kufanikisha timu hiyo kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2014
Mchezaji wa Japan Keisuke Honda akifunga mkwaju wa penalti katika mchezo dhidi Australia na kufanikisha timu hiyo kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2014
Matangazo ya kibiashara

Mabingwa hao wa Bara la Asia wanatarajia kuwa miongoni mwa timu zitakazoshiriki kwenye Mashindano ya Kombe la Mabara ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea Kombe la Dunia mwaka 2014.

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Japan raia wa Italia Alberto Zaccheroni amesema baada ya kupata tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia kwa sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye mchuano huo wa Kombe la Mabara.

Japan imeahidi kutumia Mashindano ya Kombe la Mabara kama sehemu ya kuangalia mapungufu yao kabla ya kufanyika kwa Mchuano wa Kombe la Dunia wakiwa wamejiapiza kufanya vizuri kwenye mashindano ya mwaka ujao.

Zaccheroni amesema uwepo wa wachezaji wenye umri mdogo kwenye kikosi cha Japan kunampa matumaini ya kufanya vizuri katika mashindano ya Kombe la Mabara na hata Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka 2014.

Japan ilifanikiwa kukata tiketi ya Kombe la Dunia mwaka nchini Brazili katika mchezo dhidi ya Australia uliokuwa na upinzani mkubwa kutokana na pande zote kuhitaji ushindi katika mtanange huo.

Australia ilikuwa ya kwanza kupata goli kabla ya Japan haujasawazisha kwa kupitia mkwaju wa penalti uliowekwa kimiani na Keisuke Honda kitu ambacho kiliamsha shamra shamra miongoni mwa mashabiki wa timu hiyo.

Timu ya Taifa ya Japan itakayoshiriki kwenye Mashindano ya Kombe la Mabara inatajwa itawajumuisha wachezaji mahiri wanaocheza Barani Ulaya akiwemo Shinji Kagawa kutoka Manchester United na Shinji Okazaki anayekipiga Stuttgart.

Japan imepangwa Kundi A kwenye Mashindano ya Kombe la Mabara ikiwa pamoja na wenyeji Brazil, Mabingwa wa Ulaya ni Italia sambamba na Mabingwa wa Amerika ya Kaskazini Mexico.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.