Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Klabu ya Chelsea yamtangaza Jose Mourinho kuwa Kocha Mpya na kumpa mkataba wa miaka minne kuhudumu Stamford Bridge

Klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza imethibitisha Jose Mourinho atakuwa kocha mpya wa timu hiyo kwa msimu ujao baada ya kuingia naye mkataba wa miaka minne ikiwa ni mara yake ya pili kurejea Stamford Bridge. Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu ya Chelsea Ron Gourlay ndiye amethibitisha kurudi kwa Mourinho kuinoa Chelsea kwa mara ya pili kuanzia msimu ujao baada ya kufanyakazi ya mafanikio hapo awali.

Jose Mourinho ametangazwa kuwa Kocha Mpya wa Chelsea ikiwa ni mara yake ya pili kuifundisha timu hiyo
Jose Mourinho ametangazwa kuwa Kocha Mpya wa Chelsea ikiwa ni mara yake ya pili kuifundisha timu hiyo
Matangazo ya kibiashara

Mourinho anarejea Staford Bridge baada ya kuhudumu tangu mwaka 2004 hadi 2007 alipoondoka baada ya kufikia makubaliano na Uongozi wa Chelsea kuiacha timu hiyo baada ya kuipa taji la kwanza la ligi baada ya miaka hamsini.

Gourlay amesema wameamua kumrejesha Mourinho kutokana na kutambua kazi yake nzuri na wanahitaji kupata Meneja kama yeye ili kuhakikisha timu hiyo inasonga mbele na kujipatia maendeleo na mataji zaidi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chelsea ameweka bayana Mourinho pekee ndiye anaweza akafanikisha kutimizwa kwa ndoto za klabu hiyo kuweza kupata mafanikio zaidi katika michuano mbalimbali wanayoshiriki.

Mourinho mwenye umri wa miaka 50 kutangazwa kwake kurejea tena kuinoa Chelsea kunamaliza uvumi uliokuwa umezagaa ya kwamba huenda angepewa mkataba wa kuinoa timu hiyo juma lijalo.

Mourinho ambaye anatambulika kama Special One ni kocha mwenye mbwembwe nyingi na anarejea nchini Uingereza akitokea Uhispania alikokuwa anainoa Real Madrid iliyoamua kuachana naye baada ya kumaliza msimu huu bila taji lolote.

Real Madrid iliamua kufikia makubaliano ya kuachana na Mourinho baada ya kushindwa kutimiza malengo yaliyokuwa yanatarajiwa na Klanu katika msimu huu kitu ambacho kimemfanya aondoke.

Mourinho anachukua nafasi ya Kocha wa Mpito wa Cheslea Rafael Benitez aliyejiunga na Napoli baada ya kuifanikisha timu hiyo kutwaa taji la Kombe la Europa lakini ameonekana si chaguo sahihi la kuendelea kusalia Stamford Bridge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.