Pata taarifa kuu
TENNIS-MADRID OPEN

Murray na Nadal wasonga mbele katika Mashindano ya Madrid Open huku Federer akiondoshwa mapema

Mashindano ya Tennis ya Madrid Open yameendelea kuchanja mbuga na kushuhudia wakongwe kwenye mchezo huo wakizidi kuondolewa huku wengine wakisonga mbele kutinga hatua ya mzunguko wa nne. Andy Murray na Rafael Nadal wamefanikiwa kutinga hatua ya mzunguko wa nne huku wakishuhudia Roger Federer akikumbana na kichapo cha kushtua na hivyo kuondoshwa kwenye mashindano hayo.

Andy Murray akiwa katika Mashindano ya Madrid Open akikabiliana na Gilles Simon
Andy Murray akiwa katika Mashindano ya Madrid Open akikabiliana na Gilles Simon
Matangazo ya kibiashara

Murray amefanikiwa kutinga hatua ya mzunguko wa nne wa Mashindano ya Madrid Open baada ya kumuondosha Gilles Simon kwa kumfunga raia huyo wa Ufaransa kwa seti mbili kwa moja.

Simon ndiye aliyeanza kwa kushinda seti ya kwanza kwa sita mbili kabla ya Murray kuzinduka katika seti ya pili na kushinda kwa sita nne kabla hajamaliza mchezo huo kwa kushinda seti ya tatu kwa 7-6.

Wakati Murray akikenua kwa kicheko baada ya kusonga mbele mwenzake Federer aliondoshwa kwenye mashindano hayo na mchezaji namabri kumi na nne kwenye ubora wa Tennis duniani Kei Nishikori.

Nishikori ameshinda kwa seti mbili kwa moja huku akianza kwa kushinda seti ya kwanza kwa sita kwa nne kabla ya Federer hajazinduka usingizini na kushinda seti hiyo kwa sita kwa moja lakini akafungwa katika seti ya tatu kwa sita kwa mbili.

Nadal ambaye amerejea kwa nguvu baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na kukabiliwa na maumivu amefanikiwa kudonga mbele baada ya kupata ushindi dhidi ya Mikhail Youzhny kwa kumfunga seti mbili pia.

Nadala amefanikiwa kushinda mchezo huo kwa kutopata uspinzani mkubwa baada ya kushinda seti ya kwanza kwa sita mbili kabla hajashinda katika seti ya pili kwa sita kwa tatu na kupata tiketi ya kuingia mzunguko wa nne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.