Pata taarifa kuu
Footbal

Mechi za marudio ya kalbu bingwa barani Ulaya

Mmiliki wa klabu ya soka ya Malaga kutoka nchini Uhispania Sheikh Abdullah Al-Thani analitaka shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kuchunguza ushindi wa klabu ya Dortmund Borrusia ya Ujerumani wa mabao 3 kwa 2 katika mchuano wa duru ya pili ya robo fainali katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Klabu ya Dortmund ilifuzu nusu fainali baada ya kupata ushindi huo ndani ya sekunde 70 ya muda wa ziada, mabao ambayo rais huyu wa Malaga anaona alionewa na wachezaji wake kubaguliwa kwa rangi.

Kumetokea kwa malumbano kuhusu mabao hayo mawili ya Marco Reus na Felipe Santana ambayo yalionekana kufungwa baad aya wachezaji hao kuotea.

Al-Thani amewapongeza wachezaji wake kwa kile anachokisema walishinda mchuano huo uwanjani lakini hawakutendewa haki.

Katika mchuano mwingine iliochezwa jana,licha ya ushindi wa klabu ya Galatasaray ya Uturuki wa mabao 3 kwa 2 dhidi ya Rela Madrid,vijana Jose Mourihno wamefuzu katika nusu fainali kutokana na ushindi wao wa duru ya kwanza kwa mabao 3 kwa 0.

Leo usiku michuano mingine ya robo fainali inachezwa Barcelona ya Hispania watakuwa wenyeji wa Paris Saint Germain kutoka Ufaransa katika uwanja wao wa Camp Nou.

Timu hizo mbili zilitoka sare ya mabao 2 kwa 2 katika mchuano wa duru ya kjwanza wiki iliyopita na yeyeopte atakayepata ushindi atafuzu.

Jevuntus ya Italia nayo itakuwa katika uwanja wake wa nyumbani kumenyaha na Bayern munich ya Ujerumani.

Jevuntus ambao ni mabingwa wattezi wa ligi kuu ya soka nchini Italia wanastahili kupata ushindi wa zaidi ya mabao 3 kwa bila usiku huu ili kufuzu katika awamu ya nusu fainali baada ya kufungwa na Bayern munich wiki iliyopita mabao 2 kwa 0 katika mchuano wa awamu ya kwanza.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.