Pata taarifa kuu
UEFA-UHISPANIA

Real Madrid yakaribia Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya huku Malaga na Borussia Dortmund ngoma ikiwa ngumu

Michezo miwili ya mwisho ya kukamilisha mkondo wa kwanza wa hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya imekamilika kwa kupigwa usiku wa jana na kushuhudia miamba minne ikichuana vikali.

Wachezaji wa Real Madrid wakishangilia goli la kwanza lililofungwa na Cristiano Ronaldo
Wachezaji wa Real Madrid wakishangilia goli la kwanza lililofungwa na Cristiano Ronaldo
Matangazo ya kibiashara

Real Madrid wakiwa nyumbani Santiago Bernabeu wakafanikiwa kuchomoza na ushindi mnono wa magoli 3-0 dhiid ya Galatasaray na kuonesha njia ya kuelekea hatua ya Nusu Fainali imeiva kwa upande wao.

Cristiano Ronaldo ndiyo alikuwa wa kwanza kufunga goli kwa Real Madrid katika dakika ya tisa ya mchezo huo akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Kiungo Mesut Ozil aliyemtolea pasi akiwa amesalia la mlinda mlango.

Goli hilo lilizidisha kasi ya Real Madrid na kunako dakika ya thelathini na tisa Mshambuliaji wa Kimataifa wa Ufaransa Karim Benzema akakwamisha mpira wavuni akiunganisha krosi iliyopigwa na Michael Essien.

Licha ya kufungwa magoli hayo mawili wachezaji wa Galatasaray waliendelea kucheza kwa kujiamini na kupoteza nafasi nzuri kupitia Didier Drogba, Emmanuel Eboue na Kiungo Wesley Sneijder.

Dakika arobaini na tano za kwanza zilimalizika huku vijana hao wanaonolewa na Kocha mwenye mbwembwe nyingi Jose Mourinho wakiongoza kwa magoli hayo mawili kwa nunge.

Kipindi cha pili Galatasaray walijitahiid kusaka goli la unene lakini waligonga mwamba na juhudi zilizimwa baada ya Real Madrid kupata goli la tatu lililofungwa kwa kichwa na Gonzalo Higuain.

Mchezo mwingine wa Robo Fainali ya kwanza ulishuhudia miamba miwili Malaga na Borussia Dortmund wakichoshana nguvu katika mchezo mwingine uliopigwa katika dimba la La Rosaleda.

Dortmund walionekana kuwa na uchu kusaka ushindi kwa udi na ubani lakini juhudi zao ziliishia kwenye miko ya mllinda mlango wa Malaga Willy aliyeokoa michomo ya washambuliaji wa timu hiyo ya Ujerumani.

Mario Gotze na Robert Lewandowski walionekana kuwa na uchu wa kuzifumania nyavu za wapinzani wao Malaga lakini hawakufanikiwa kutokana na umahiri na umakini wa mlinda mlango wa Malaga.

Malaga walitengeneza nafasi chache ukilinganisha na wageni wao Dortmund ambao wanaonekana walienda La Rosaleda kwa lengo la kusaka goli la ugenini lakini wamejikuta wakigonga mwamba.

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kupigwa juma lijalo nchini Ujerumani huku Dortmund wakiwa na wakati mgumu kutokana na kutakiwa kutoruhusu goli kutoka kwa wapinzani wao Malaga kama wanataka kutinga hatua ya Nusu Fainali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.