Pata taarifa kuu
UTURUKI-UINGEREZA-UHISPANIA

Mshambuliaji wa Galatasaray Didier Drogba anaamini Jose Mourinho atarejea Uingereza kukinoa Kikosi cha Chelsea

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Cote D'Ivoire anayekipiga katika Klabu ya Galatasaray ya Uturuki Didier Drogba amesema anaamini Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho huenda akarejea na kukinoa Kikosi cha Chelsea maarufu kama The Blues. Drogba ametoa kauli hiyo wakati huu ambapo Galatasaray inatarajiwa kushuka dimbani usiku wa leo kukabiliana na Real Madrid kwenye mchezo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Mshambuliaji wa Galatasaray Didier Drogba akiwa anawajibika uwanjani
Mshambuliaji wa Galatasaray Didier Drogba akiwa anawajibika uwanjani
Matangazo ya kibiashara

Nahodha huyo wa Timu ya Taifa ya Cote D'Ivoire amesema kile ambacho kinamsukuma aamini Mourinho atarejea Stamford Bridge ni kutokana na uwepo wa kitu ambacho hajakimaliza kwenye kazi yake.

Drogba ambaye ameshawahi kuwa chini ya Mourinho wakati akikipigana The Blues amesema hafikirii kama kocha huyo mwenye mbwembwe nyingi ameshamalizana na Chelsea.

Mshambuliaji huyo aliyefunga penalti ya mwisho kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani ulaya kati ya Chelsea na Bayern Munich anasema kazi ambayo haijakamilishwa na Mourinho ni kushinda taji hilo akiwa na The Blues.

Drogaba amewaambia wanahabari ameshawishika kusema hivyo kutokana na Mourinho kushinda mataji yote nchini Uingereza ikiwa ni pamoja na Ligi mara mbili lakini kitu ambacho hakushinda na The Blues ni Kombe la Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Mshambuliaji huyo wa Galatasaray aliyejiunga akitokea China katika Klabu ya Shanghai Shenhua amemsifu Mourinho kwa kusema ni mtu ambaye amekuwa karibu sana na wachezji kitu kinachochangia mafanikio yake.

Drogba amesema ipo siku Mourinho atarejea Stamford Bridge kutokana na licha ya kuzifuza Inter Milan na Real Madrid lakinio bado amekuwa akiiongelea Chelsea kila mara anapohojiwa.

Katika hatua nyingine kueleka mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya Kocha wa Real Madrid Mourinho amekataa kuzungumzia hatima yake ya baadaye katika timu hiyo yenye maskani yake Santiago Bernabeu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.