Pata taarifa kuu
EUFA-UJERUMANI-UFARANSA

Bayern Munich yaizima Juventus kwenye mkondo wa kwanza wa Robo Fainali huku Barcelona ikibanwa mbavu na PSG

Klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani imejiweka katika mazingira mazuri ya kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya baada ya kufanikiwa kuchomoza na ushindi kwenye mkondo wa kwanza wa hatua ya Robo Fainali.

Mshambuliaji wa Bayern Munich Thomas Mueller akifunga goli la pili dhidi ya Juventus
Mshambuliaji wa Bayern Munich Thomas Mueller akifunga goli la pili dhidi ya Juventus
Matangazo ya kibiashara

Bayern Munich wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Juventus kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Allianz Arena na kujiweka katika nafasi nzuri kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa juma lijalo.

Beki wa kushoto wa Munich David Alaba alikuwa wa kwanza kuiba uongozi klabu yake baada ya kufunga goli la kwanza sekunde 30 tangu kuanza kwa mchezo huo kwakufyatua mkwaju umbali wa mita 35.

Goli hilo lilidumu hadi dadkika 45 za kwanza zinamaliza lakini Bayern Munich walirejea kipindi cha pili wakiwa na hasira zaidi na kufanikiwa kupata goli la pili lililofungwa na Thomas Mueller akimaliza kazi nzuri iliyofanywa na Mario Mandzukic.

Kipa wa Bayern Munich Manuel Neuer alilazimika kufanyakazi ya ziada mara mbili kuokoa michomo ya Arturo Vidal aliyekuwa mwiba kwenye safu ya ulinzi ya timu hiyo lakini Juventus imesema itajipanga kwa mchezo wa marudiano.

Mchezo mwingine wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya ulishuhudia Paris St-Germain na Barcelona wakienda sare ya magoli 2-2 na sasa mchezo wa pili utakaopingwa Nou Camp ndiyo utaamua nani anatinga nusu fainali.

Barcelona ilikuwa ya kwanza kupata goli katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Parc Des Princes kupitia mchezaji bora mara nne wa dunia Lionel Messi akiiunganisha pasi mwanana iliyopigwa na Dani Alves.

Goli hilo lilidumu hadi dakika 45 za kwanza zilipotamatika lakini kipindi cha pili PSG wakiwatumia wachezaji wao mahiri kama David Beckham walifanikiwa kusawazisha kupitia mchezaji wa zamani wa Barcelon Zlatan Ibrahimovic.

Mesii alishindwa kumaliza mchezo huo baada ya kuumia nyama za paja na kualazimika kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Cesc Fabregas lakini mabadiliko ambayo hayakuleta kitu kipya sana.

Barcelona walipata goli la pili kwa mkwaju wa penalti baada ya mlinda mlango wa PSG Salvatore Sirigu kumuangusha Alexis Sanchez na mwamuzi kuamuru ipigwe penalti iliyoweka kimiani na Xavi Hernandez.

PSG waliendelea kulishambulia lango la Barcelona ambao waliamini goli lao la dakika ya 89 lingetosha kuwapa ushindi na kunako dakika nne za ziada wakafanikiwa kusawazisha kupitia Blaise Matuidi ambaye atakosa mchezo wa marudiano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.