Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Kocha wa Chelsea Benitez asisitiza kipaumbele chake ni kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye Ligi Kuu

Kocha wa Muda wa Chelsea Rafael Benitez ameendelea kusisitiza lengo lake ni kuhakikisha timu yake inamaliza katika nafasi juu nne katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza.

Kocha wa muda wa Chelsea Rafael Benitez akiwajibika wakati timu yake ikiwa dimbani
Kocha wa muda wa Chelsea Rafael Benitez akiwajibika wakati timu yake ikiwa dimbani REUTERS/Andrew Winning
Matangazo ya kibiashara

Benitez amesema hicho ndiyo kipaumbele chao ili waweze kupata nafasi ya kufuzu kushiriki mashindano ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao licha ya kukabiliwa na upinzani kutoka kwa Tottenham na Arsenal.

Kocha huyo wa Muda ametoa kauli hiyo baada ya kushuhudia Chelsea ikitinga nusu fainali ya Kombe la Chama Cha Soka FA baada ya kuizaba Manchester United kwa goli 1-0 kwenye mchezo wa marudiano uliopigwa Stamford Bridge.

Benitez amesema licha ya kamba ushindani umekuwa mkubwa sana wa kupata nafasi hizo nne za juu lakini wataendelea kupambana hadi mwishoni mwa msimu na kuhakikisha wanapata nafasi hizo.

Kocha huyo aliyewahi kuinoa Liverpool ameweka bayana mbio za kusaka nafasi ya tatu au ya nne ni ngumu sana kutokana na kila timu ambacho ipo kwenye nafasi ya kuwepo kuendelea kujiimarisha kuhakikisha wanashiriki kwenye Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Benitez amesema licha ya timu yake kuwa katika hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Europa na Nusu Fainali ya Kombe la FA lakini bado wanakibarua kigumu mbele yao kuhakikisha wanatimiza malengo yao.

Chelsea ambayo imesalia na michezo miwili kabla ya kufanikiwa kutetea Ubingwa wa Kombe la FA na iwapo watashinda litakuwa taji lao la tano katika kipindi cha misimu saba ya mashindano hayo.

Chelsea ni timu ambayo imecheza michezo 29 ya Kombe la FA bila ya kufungwa na kuweka rekodi ya kucheza michezo mingi zaidi bila ya kufungwa huku mataji yao wakiyachukuwa mwaka 2007, 2009, 2010 na 2012.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.