Pata taarifa kuu
SOKA

Vijana wa DRC wasiozidi umri wa miaka 20 watoka sare ya kutofungana na Gabon michuano ya Afrika

Timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yenye chini ya umri wa miaka 20 walitoka sare ya kutofungana na Gabon na kupata alama moja katika mechi ya kwanza ya kundi la pili katika michuano ya kuwania ubingwa wa Afrika inayoendelea jijini Algers nchini Algeria.

Matangazo ya kibiashara

Gabon walionesha kiwango cha juu cha mchezo huo  na kuutawala lakini wakashindwa kupata bao dhidi ya vijana chipukizi wa Leopard ambayo inawakilisha DR Congo katika mashindano haya kwa mara ya kwanza.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilikosa bao baada ya shuti la Leandre Sombelta kulenga goli na kuokolewa na kipa Diafuka.

DR Congo ni ya pili katika kundi la pili kwa alama 1 huku Mali ikiongoza kwa alama 3 baada ya kuishinda Nigeria 1 kwa 0 katika mchuano wa ufunguzi mwishoni mwa juma lililopita.

Kundi la kwanza linaoongozwa na Misri ambayo ina alama tatu baada ya kuishinda Ghana mabao 2 kwa 1 huku wenyeji Algeria wakitoka sare yaya kutofungana na Benin.

Siku ya Jumanne Ghana itamenyana na Benin huku Algeria ikichuana na Misri.

Jamhuri ya Kidemokarsia ya Congo itachuana na Mali katika mchuano wa pili huku Nigeria ikicheza na Gabon.

Timu nne zitakazofika katika hatua ya nusu fainali zitashiriki katika kombe la dunia nchini Uturuki kati ya mwezi Juni na Julai mwaka huu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.