Pata taarifa kuu
AFCON 2013

Ivory Coast yaifunga Togo, wakati Tunisia ikiifunga Algeria, leo ni zamu ya wenyeji Afrika Kusini dhidi ya Angola, Morocco na Cape Verde

Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika imeendelea kushika kasi nchini Afrika Kusini ambapo timu za kundi D zilionyeshana ubabe kwenye mechi zilizochezwa siku ya Jumanne. 

Mchezaji wa Togo, Jonathan Ayitea akishangilia bao la kusawazisha alilofungia timu yake, Togo ilifungwa 2-1 na Ivory Coast
Mchezaji wa Togo, Jonathan Ayitea akishangilia bao la kusawazisha alilofungia timu yake, Togo ilifungwa 2-1 na Ivory Coast Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katika mchezo wa awali Tembo wa Ivory Coast, timu ya taifa ya nchi hiyo, ilikuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Togo kwenye mchezo ambao umeshuhudia Ivory Coast wakichomoza na ushindi wa mabao 2-1.

Walikuwa ni Ivory Coast ambao walikuwa wa kwanza kuandika bao kupitia kwa Yaya Toure kabla ya Togo krejesha goli hilo kupitia kwa mchezaji wake Jonathan Ayite.

Katika kipindi cha kwanza Togo walikosa nafasi nyingi za wazi ambazo pengine zingeiwezesha timu hiyo kuibuka na ushindi ambapo mchezaji wake Emmanuel Adebayor alikosa magoli ya wazi.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo walikuwa ni Ivory Coast kwa mara nyingine ndio waliokuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza kupitia kwa mchezaji wake Gervinho anayekipiga na klabu ya Arsenal.

Katika mchezo mwingine uliwakutanisha mahasimu wa Afrika Kaskazini timu ya taifa ya Tunisia ambayo ilikuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Algeria kwenye mchezo ambao umeshuhudia Tunisia wakiibuka na ushindi wa bao 1-0.

Hii leo kutakuwa na michezo ya kundi A ambapo wenyeji wa michuano hiyo Afrika Kusini ambao mchezo wa awali walitoka sare na Cape Verde watakuwa na kibarua dhidi ya Angola kwenye mchezo mwingine ambao Afrika Kusini wako kwenye shinikizo la mashabiki wao kutaka ishinde.

Katika mtanange mwingine Cape Verde watakuwa na kibarua dhidi ya Morocco kwenye mchezo mwingine ambao unatarajiwa kuwa mgumu kwa timu zote mbili kutokana na aina ya mchezo wa timu hizo mbili kufanana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.