Pata taarifa kuu
Gabon

Emmanuel Adebayor aamua kuichezea Timu yake ya Taifa nchini Afrika kusini

Hatimaye mshambulizi wa kimataifa wa Togo katika mchezo wa soka Emmanuel Adebayor ameamua kuichezea timu yake ya taifa katika mashindano ya kutafuta ubingwa wa Afrika nchini Afrika Kusini yatakayoanza tarehe 19 mwezi huu.

Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Togo,Emmanuel Adebayor
Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Togo,Emmanuel Adebayor REUTERS/Suzanne Plunkett
Matangazo ya kibiashara

Awali Adebayor alisusia kuichezea nchi yake kwa kile alichokisema maswala ya kiusalama na pia wachezaji kutolipwa marupurupu yao na shirikisho la soka nchini humo.
 

Tayari mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 28 amejiunga na wenzake nchini Ghana wanakojiandaa kwa michuano hiyo ambayo wamepangwa katika kundi moja na Cote Dvoire, Algeria na Tunisia.
 

Shirikisho la soka nchini Togo lilikuwa limempa Adebayor hadi baadaye juma hili kuamua ikiwa angeichezea timu ya taifa au la kabla ya kutajwa kwa kikosi cha mwisho.
 

Kuondoka kwa Adebayor katika klabu yake ya Totenham Hotspurs nchini Uingereza kumeacha mwanya ambao sasa Jermain Defoe atalazimika kuuziba kwa kipindi cha mwezi mmoja ambacho Adabayor atakuwa nchini Afrika Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.