Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Balotelli ataka kuzichapa kavu kavu na Kocha wake Mancini kwenye uwanja wa mazoezi

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Italia ambaye anakipiga katika Klabu ya Manchester City Mario Balotelli ameendeleza utukutu wake baada ya kutaka kupiga na Kocha wake Roberto Mancini kwenye Uwanja wa Mazoezi. Balotelli na Mancini walitaka kupigana kavu kavu kutokana na Kocha huyo kukwera na namna ambavyo alimchezea vibaya mchezaji mwenzake Scott Sinclair kwenye mazoezi ya kawaida wa timu hiyo.

Kocha Mkuu wa Manchester City Roberto Mancini akiwa amemkunja shati Mshambuliaji wake Mario Balotelli
Kocha Mkuu wa Manchester City Roberto Mancini akiwa amemkunja shati Mshambuliaji wake Mario Balotelli
Matangazo ya kibiashara

Picha zilizopigwa kwenye tukio hilo zinaonesha namna ambavyo Mancini alivyomvaa mwilini Balotelli ambaye naye hakuonekana kuwa mpole kwenye tukio hilo ambalo linaongeza wasiwasi wa yeye kuwepo kwenye kikosi cha Manchester City.

Makocha Wasaidizi wa Manchester City ndiyo ambao waliingilia kati na kuwatenganisha Balotelli na Mancini huko Kocha huyo akionekana amefura kwa hasira kutokana na tabia mbaya ya Mshambulizji wake huyo kipenzi.

Makocha wengi wanejikuta wakitamka pasi na ubishi kwa tabia ambayo inaoneshwa na Balotelli huenda akawa na mwisho mbaya kwenye soka licha ya kuwa mchezaji kinda mwenye kipaji cha hali ya juu katika kusaka kabumbu.

Hii ni mara nyingine tena kwa Balotelli kutawala vichwa vya habari kwa ukorofi wake kwenye mazoezi ya Manchester City kwani hapo awali ameshazichapa na wachezaji wenzake akiwemo Kollo Toure.

Balotelli mchezaji mwenye vituko vya mara kwa mara na ukorofi uliopindukia amekuwa akijiona kama mchezaji ambaye anaandamwa zaidi kutokana na tabia yake kuwakera wengi na amekuwa kaidi kubadilika.

Kocha Mkuu wa Manchester City Mancini anatarajiwa kutoa ukweli wa suala hilo pale ambapo atakuwa kwenye mkutano na waandishi wa habari baadaye hii leo akieleza mchezo wao wa Kombe la FA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.