Pata taarifa kuu
UINGEREZA

QPR yaanza Mwaka Mpya kwa ushindi wa Ligi Kuu Nchini Uingereza dhidi ya Chelsea

Klabu ya Queens Park Rangers ambayo inapambana kujiepusha na baa la kushuka daraja kwenye Ligi Kuu Nchini Uingereza hatimaye imeuanza mwaka 2013 kwa ushindi baada ya kuwafunga Mabingwa watetezi wa Kombe la FA Chelsea. QPR imepata ushindi wa ugenini kwenye Dimba la Stamford Bridge kwa goli moja kwa nunge na hivyo kuanza harakati zake vyema za kujinasua na eneo la hatari la kushuka daraja msimu huu.

Wachezaji wa QPR wakishangilia goli lililofungwa na Shaun Wright-Phillips dhidi ya Chelsea
Wachezaji wa QPR wakishangilia goli lililofungwa na Shaun Wright-Phillips dhidi ya Chelsea
Matangazo ya kibiashara

Goli la pekee la QPR liliweka kimiani na Mshambuliaji wake Shaun Wright-Phillips ambaye alitokea benchi baada ya kuwa majeruhi na kukosa michezo kadhaa ya mwishoni mwa mwaka jana.

QPR imefanikiwa kusitisha rekodi nzuri ya Chelsea ambayo ilikuwa imeshinda michezo mitano mfululizo lakini kichapo hicho kinaonekana kikwazo cha mbio za The Blues kwenye kusaka ubingwa wa mwaka huu.

Mlinda mlango wa QPR Julio Cesar alionekana kufanya kazi kubwa kwa kuokoa michomi mingi ya washambulizji wa Chelsea akiwemo Fernando Torres aliyeonekana kuwa na uchu mkubwa wa magoli.

Chelsea almanusura wapate goli la kuongoza kupitia Kiungo wao Frank Lampard lakini mwamuzi wa mchezo huo alilikataa kutokana na mchezaji kuwepo eneo lililochangia kuharamisha goli hilo.

QPR licha ya ushindi huo uliowashtua wengi lakini bado imeendelea kusalia mkiani mwa Ligi Kuu nchini Uingereza wakiwa amejikuzanyia pointi kumi na tatu pekee kwenye michezo yao ishirini na moja.

Kocha Mkuu wa QPR Harry Redknapp alipongeza namna ambavyo kikosi chake kimecheza na kusema lengo lao ni kuhakikisha wanaondoka kwenye eneo la kushuka daraja na kuweza kusalia kwenye msimu ujao.

Rafael Benitez ambaye ni Kocha wa muda wa Chelsea kwa upande wake ametoa sababu ya kupata kipigo hicho ni kupumzisha baadhi ya wachezaji ambao wanaonekana kuchoka kutokana na kucheza mechi mfululizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.