Pata taarifa kuu
Barcelona

Lionel Messi aweka rekodi katika ufungaji wa mabao

Mchezaji wa Kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona nchini Uhispania Lionel Messi ameweka historia kwa kufunga mabao 86 mwaka 2012 katika mechi zote alizoichezea  klabu yake na timu yake ya taifa.

Matangazo ya kibiashara

Messi amevunja rekodi ya Gerd Mueller kutoka Ujerumani aliyeweka Historia kama hiyo mwaka 1972 kwa kufunga mabao 85.

Historia hiyo imeandikwa baada ya Messi kufunga mabao mawili mwishoni mwa wiki iliyopita katika mechi ya ligi kuu ya soka nchini Uhispania kwa kuifunga Real Betis mabao 2 kwa 1.

Mbali na rekodi hiyo, Messi pia anakumbukwa sana kushinda taji la mchezaji bora mara tatu mfululizo ikiwemo mwaka uliopita.

Messi anatarajiwa kuendeleza rekodi yake ya ufungaji wa mabao katika klabu yake ya Barcelona wakati klabu hiyo itakapocheza na Benfica FC ya Ureno katika michuano ya kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya.

Mshambulizi huyo matata ameifungia klabu ya Barcelona mabao 74 tangu aanze kuichezea timu hiyo na Argentina mabao 12.

Lionel Messi pia amejumuishwa kuwania taji la mchezaji bora mwaka huu na yeye anasema lengo lake kuu si kuweka historia bali ni kuisaidia timu yake kunyakua mataji.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.