Pata taarifa kuu
UEFA CHAMPIONS LEAGUE

Benitez: Chelsea hatujakata tamaa, tutawania taji la Europa

Kocha mkuu wa waliokuwa mabingwa watetezi wa kombo la klabu bingwa barani Ulaya, Rafa Benitez amesema kuwa timu yake kwasasa inalenga kutwaa taji la Europa League baada ya kutupwa nje kwenye Champions League.

Kocha mkuu wa timu ya Chelsea, Rafa Benitez
Kocha mkuu wa timu ya Chelsea, Rafa Benitez Reuters
Matangazo ya kibiashara

Benitez ametoa kauli hiyo mara baada ya kushuhudia timu yake ikiaga mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya licha ya ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya klabu ya FC Nordsjælland.

Benitez ambaye toka aichukue klabu hiyo toka kwa Roberto De Mateo amekuwa akikabiliwa na upinzani mkali toka kwa mashabiki wa timu hiyo ambao wameonesha wazi kutokuwa na imani na kocha huyo kwa madai kuwa hana uwezo wa kuiletea mataji timu hiyo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mechi yake Benitez amesema sasa wanaelekeza nguvu zao katika kuhakikisha wanajaribu kunyakua kombe la Europa ili kuleta faraja kwa mashabiki wa timu hiyo.

Kauli ya Benitez inalinga na ile ya kocha wa Manchester City Roberto Mancin ambaye mara baada ya kushuhudia timu yake ikitolewa kwenye UEFA na kisha kushindwa kupata nafasi ya kufuzu kwenye Europa, ameelekeza nguvu zake katika kutaka kutetea taji la ligi kuu ya nchini Uingereza.

Mechi zingine zilizopigwa hiyo jana ni pamoja na Manchester United wakiwa nyumbani walikubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa klabu ya FC Cluj, wakati Braga wakikubali kipigo cha mabao 2-1 toka kwa Galatasaray.

Mtanange mwingine ulikuwa ni ule kati ya klabu ya Juventus waliokuwa na kibarua dhidi ya timu ya Shakhtar Donetsk, kwenye mchezo ambao Juve walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao 1-0.

FC Barcelona wao walijikuta wakilazimishwa sare ya bila kufungana na klabu ya Benfica kwenye mchezo ambao ulishuhudia mshambuliaji hatari wa Barca Leonel Messi akipata majeraha ya goti yaliyosababisha atolewe nje na machela.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.