Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Chelsea yatinga Robo Fainali ya Kombe la Carling huku Bingwa Mtetezi Liverpool akiondolewa

Klabu ya Chelsea imefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya michunao ya Catling baada ya kufanikiwa kuifunga Manchester United kwa magoli 5-4 ikiwa ni kama kulipiza kisasi baada ya kukubali kipigo cha magoli 3-2 katika mchezo wa Ligi uliopigwa siku ya jumapili.

Wachezaji wa Chelsea wakishangilia goli lililofungwa na Daniel Sturridge kwenye mchezo dhidi ya Manchester United
Wachezaji wa Chelsea wakishangilia goli lililofungwa na Daniel Sturridge kwenye mchezo dhidi ya Manchester United
Matangazo ya kibiashara

Manchester ikiwa imefanya mabadiliko ya wachezaji wake tisa ambao walianza kwenye kikosi kilichopata ushindi mbele ya Chelsea siku ya jumapili kializa vyema mchezo huo na kuwa wa kwanza kupata goli lililofungwa na Mkongwe Ryan Giggs.

Chelsea walifanikiwa kusawazisha goli hilo kupitai mkwaju wa penalti ambao uliwekwa kimiani na Davis Luiz kabla ya Javier Hernandez hajapachika goli la pili kutokana na kuwazidi ujanja mabeki wa The Blues.

Kipindi cha pili Chelsea ilisawazisha kupitia Gary Cahill kabla ya Manchester kuongoza kwa mara ya tatu kupitia goli lililofungwa kiufundi na Luis Nani lakini mchezo ukielekea mwishoni The Blues walizawadiwa penalti katika dakika za nyongeza na Eden Hazard akafunga.

Dakika thelathini za nyonge zailishuhudia Chelsea ikipata magoli mengine mawili kupitia Daniel Sturridge na Ramimes huku Giggs akifunga goli la nne kwa upande wa Mashetani Wekundu na mchezo kumalizika kwa matokeo hayo.

Katika mchezo mwingine Mabingwa watetezi wa Kombe la Carling Liverpool wamekubali kichapo cha magoli 3-1 kutoka kwa Swansea ambao walipata magoli yao kupitia kwa Chico Flores, Nathan Dyer na Jonathan De Guzman.

Vijogoo vya Jiji Liverpool walipata goli lao la kufutia machozi kupitia mshambuliaji wake Luis Suarez ambaye aliingia kipindi cha pili pamoja na Steven Gerrard na Raheem Sterling lakini wakashindwa kuikoa timu yao na kipigo.

Tottenham nao wakayaaga mashindano hayo baada ya kupata kichapo cha kushutukiza cha magoli 2-1 kutoka kwa Norwich City ambao walitoka nyuma na kupata ushindi huo uliowapeleka hatua ya robo fainali.

Tottenham ndiyo ilikuwa ya kwanza kufunga kupitia kwa Gareth bale kabla ya Norwich kuamka kutoka usingizini na kujipatia magoli yao kupitia Alex Tettey na Simeon Jackson na hivyo kutinga hatua ya robo fainali.

Ratiba ya robo fainali ya Kombe la Carling inaonesha Leeds United itakuwa mwenyeji wa Cheslea wakati Arsenal italazimika kufunga safari kuwafuata Bradford huku Norwich City wakiwa nyumbani kupambana na Aston Villa na mchezo mwingine utakuwa kati ya Swansea na Middlesbrough.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.