Uingereza yaondolewa katika michuano ya Cricket ya Twenty20
Uigereza imeondolewa katika michuano ya kimataifa ya Cricket ya Twenty20 na wenyeji wao Sri Lanka baada ya kushindwa kwa mikimbio 19.
Imechapishwa:
Kushindwa kwa Ungereza kunamaliza matumaini ya timu hiyo kutinga katika hatua ya nusu fainali licha ya kupewa nafasi kubwa katika mashindano hayo baada ya kuiangusha New Zealand kwa wiketi 6 Jumamosi iliyopita.
Uzoefu wa wachezaji Samit Patel na Lasith Malinga ulisaidia sana Sri Lanka kunyakua ushindi huo baada ya wachezaji hao kupata wiketi 5 na kudidimiza kabisa matumaini ya Uingereza kusonga mbele.
Nahodha wa Ungereza Stuart Broad amekiri kuwa wachezaji wake walicheza chini ya kiwango na kusababisha kushindwa huko ambako pia kulichangiwa na ukosefu wa uzoefu wa wachezaji hao katika michuano ya kimataifa kama hii.
Sri Lanka sasa inasubiri mshindi kati ya Australia na Pakistan wanaocheza siku ya Jumanne, huku India na Afrika Kusini pia wakitarajiwa kufuzu kwa nusu fainali.