Pata taarifa kuu
UHISPANIA-UINGEREZA-UJERUMANI

Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya kuanza kutimua vumbi hii leo kwenye hatua ya makundi

Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya UEFA Champions League inatarajiwa kuanza hii leo katika hatua ya makundi ambapo klabu kumi na sita zitashuka dimbani kusaka pointi tatu muhimu kwenye viwanja vinane tofauti.

Nembo maalum ambayo inatumiwa na Chama Cha Soka Barani Ulaya kwa jili ya Mashindano ya Ligi ya Mabingwa
Nembo maalum ambayo inatumiwa na Chama Cha Soka Barani Ulaya kwa jili ya Mashindano ya Ligi ya Mabingwa © UEFA
Matangazo ya kibiashara

Reald Madrid inayonolewa na Jose Mourinho ambayo imekuwa na mwanzo mbaya wa ligi kuu nchini Uhispania msimu huu itakuwa nyumbani kupambana na Manchester City ambayo imekuwa ikipambana ili kujijengea sifa kwenye mashindano hayo.

Mourinho kabla ya mchezo huo amewataka wachezaji wake kupambana kwenye mchezo huo ili kuhakikisha anapata ushindi kwani lengo lake ni kuhakikisha anashinda Ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya msimu huu.

Kocha wa Manchester City Robert Mancini amewataka wachezaji wake kucheza kwa umakini mkubwa na hatimaye kupata ushindi ambao utasaidia harakati zao za kuvuka hatua ya makundi.

Mchezo mwingine wa Kundi D utazikutanisha Borussia Dortmund dhidi ya Ajax mchezo ambao utapigwa nchini Ujerumani ambapo mabingwa hao watetezi wa Ligi ya Bundesliga watakuwa nyumbani.

Arsenal wanaonolewa na Arsene Wenger wenyewe wameelekea nchini Ufaransa kucheza na Montpellier huku wakiwa wanachagizwa na ushindi wa kwenye ligi wa magoli 6-1 dhidi ya Southampton.

Arsenal wapo Kundi B ambapo mchezo mwingine utazikutanisha Olympiakos ya Ugiriki dhidi ya Schalke 04 ya Ujerumani mchezo utaopigwa katika Jiji la Athens.

Kundi A litashuhudia Dinamo Zagreb wakipambana na FC Porto wakati vijana kutoka Ufaransa PSG wakiwa nyumbani wenyewe watakuwa na kibarua kigumu mbele ya Dynamo Kiev.

Mchezo ya Kundi C itashuhudia Malaga wakicheza dhidi ya Zenit wakati mchezo mwingine kwenye kundi hilo utashuhudia AC Milan wakichuana na Anderlecht.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.