Pata taarifa kuu
Olympiki

Senegal yafanya vizuri, wakati Morocco, Gabon zikiboronga

Wawakilishi wa Afrika katika michuano ya Olympic upande wa mpira wa miguu waendelea kuboronga huko jijini London, huku Senegal ikiwakilisha vizuri katika michuano hiyo. Simba wa Teranga wa Senegal imeishinda Uruguay mabao 2-0 katika michuano ya Olympic inayoendelea huko jijini London, wakati huo huo Misri imekwenda sare ya kufungana bao 1-1 na New Zealand katika kundi C, huku Gabon ikilambishwa mchanga na Mexico kwa mabao 2-0 katika kundi B. Wawakilishi wengine kutoka bara la Afrika Morroco imelazimika kusalimu amri mbele ya Japan kwa kipigo cha bao 1-0 katika kundi D.

Timu ya taifa ya Senegal
Timu ya taifa ya Senegal
Matangazo ya kibiashara

Timu ya Senegal ambayo ni ya nne katika michuano ya mataifa ya Afrika ya vijana wa umri chini ya miaka 23, ambayo ijiandikia tikiti ya kushiriki michuano hiyo kwa bahati sasa yao ndio yangara katika michuano hiyo ya Olympic 2012.

Baada ya kuilazimisha Uingereza sare ya bao 1-1, senegal iliokatika kundi A imejikuta kwenye nafasi ya kwanza ya kundi hilo baada ya matokeo ya ma bao 2-0 dhidi ya Uruguay licha ya mchezaji mmoja wa Senegal kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Ili kuingia katika robo fainali, Simba wa Teranga wanatakiwa angalau sare katika mechi yao na Saudia Arabia itayo chezwa Agosti Mosi.

Siku ya jana haikuwa nzuri kwa wawakilishi wengine wa Afrika Timu ya Gabon iliokwenye kundi B, Misri iliokwenye kundi C na Morroco iliokwenye kundi D. Misri ililazimishwa sare ya bao 1-1 na New Zealand, Gabon na Morocco zilipoteza mchezo

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.