Pata taarifa kuu
CRICKET

Kocha wa zamani wa Kenya wa Cricket Mike Hesson apata kazi mpya

Mike Hesson, aliyejiuzulu kama kocha wa timu ya taifa ya Cricket ya Kenya kwa kile alichosema ni kwa sababu za kiusalama ameteuliwa kama kocha wa New Zealand.

Matangazo ya kibiashara

Hesson anakuwa kocha wanne wa New Zealand ndani ya miaka minne baada ya kupigiwa upato mkubwa wa kuchukua nafasi hiyo kutokana na uzoefu wake katika mchezo huo.

Kocha huyo mpya mwenye umri wa miaka 37 anachukua nafasi ya John Wright ambaye anawaongoza kikosi cha New Zealand katika mashindano ya kimataifa huko West Indies na atakabidhi kikosi hicho mwezi ujao baada ya kukamilika kwa michuano hiyo.

Hesson alijiunga na timu ya taifa ya Kenya mwaka 2011 kabla ya kujiuzulu miezi 10 kumi baada ya  kutia saini kandarasi ya miaka miwili.

Kocha huyo alianza kushirki katika mchezo wa Cricket akiwa na miaka 22 na kuichezea timu ya taifa ya Otago kati ya mwaka 1998 hadi 2004.

Kati ya mwaka 2005 -2006 alikuwa kocha wa Otago kabla ya kujiunga na Kenya .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.