Pata taarifa kuu
Tottenham Hotspurs

Kumsajili Lukas Modric ni Pauni Milioni 35

Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs Andre Villas-Boas anawataka viongozi wa vlabu vya soka wanaomtaka kumsajili mchezaji Luka Modric watoea Pauni Milioni 35.

Matangazo ya kibiashara

Real Madrid ya Uhispania, Manchester United ya Uingereza na Paris St-Germain ya Ufaransa ni miongioni mwa vlabu ambavyo vimeonesha nia ya kumsajili mchezaji huyo raia wa Croatia.

Modric kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita, amekuwa akisema anataka kuondoka katika klabu hiyo na kocha wake Villa Boas ansema ni sharti uamuzi wake uheshimiwe.

Mchezaji huyo alijiunga na klabu hiyo ya White Hart Lane mwaka 2008 kutoka klabu ya Dinamo Zagreb ya Croatia.

Msimu uliopita akiichezea Tottenhum , Modric alicheza mechi 51 na kufunga mabao 5.

Modric mwenye umri wa miaka 26 alitarajiwa kumaliza kandarasi yake na Tottenham mwaka 2016 lakini inavyonekana huenda akaisitisha.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.