Pata taarifa kuu
SENEGAL-UINGEREZA

Timu ya Taifa ya Senegal yamhitaji Demba Cisse kutoka Newcastle United ashiriki kwenye Olimpiki

Shirikisho la Soka Nchini Senegal FSF lipo kwenye mazungumzo na Kocha Mkuu wa Klabu ya Newcastle United Alan Pardew ili kuweza kumruhusu Papiss Demba Cisse aweze kujumuishwa kwenye Timu ya Mpira wa Miguu itakayoshiriki Olimpiki.

Kocha Mkuu wa Newcastle United Alan Pardew akiwa na Mshambuliaji wake Papiss Demba Cisse raia wa Senegal
Kocha Mkuu wa Newcastle United Alan Pardew akiwa na Mshambuliaji wake Papiss Demba Cisse raia wa Senegal
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo ambayo yanaendelea kwa sasa kwa mujibu wa Pardew ni kupata ruhusa ya Papiss Demba Cisse kwenye michezo ambayo itapigwa baadaye mwezi huu katika Jiji la London nchini Uingereza.

Mazungumzo hayo hayahusiani kabisa na kumpata Demba Ba ambaye naye ni raia wa Senegal ambaye anakipiga katika Klabu ya Newcastle United na wamekuwa na mchango mkubwa kwenye timu ya taifa.

Pardew amesema kwa namna ambavyo mazungumzo hayo yanavyokwenda kuna uwezekano mkubwa wa wao kutoa ruhusa kwa Demba Cisse kushiriki kwenye michuano ya Olimpiki akiwa sehemu ya wachezaji wenye umri wa zaidi ya miaka ishirini na tatu.

Timu zote ambazo zinashiriki kwenye mashindano ya Olimpiki baadaye mwezi huu wanatakiwa wawe wamewasilisha majina ya wachezaji wao kumi na wanane ifikiapo tarehe tisa ya mwezi Julai.

Wachezaji hao wakiwa ni pamoja na watatu ambao wamezidi miaka ishirini na watatu na Senegal wanapambana kuhakikisha wanakamilisha mazungumzo na Klabu ya Newcastle United mapema kabla ya tarehe hiyo.

Kocha Mkuu wa Newcastle United Pardew anasema wanamhitaji zaidi Demba Cisse kutokana na timu hiyo kuwa na mashindano mengi mwaka huu na kutolea mfano wa wao kushiriki kwenye kombe la Europa pamoja na Ligi Kuu nchini Uingereza.

Senegal imepamgwa kundi moja na Muungano wa Uingereza, Uruguay pamoja na Umoja wa Falme za Kiarabu UAE ambapo mchezo wao wa kwanza watacheza na Muungano wa Uingereza katika Uwanja wa Old Trafford.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.