Pata taarifa kuu
LIGI YA MABINGWA ULAYA

Chelsea yaigaragaza Barcelona kwenye mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya

Nusu fainali ya pili ya ligi ya mabingwa barani Ulaya imeendelea tena jana usiku kwa mchezo mmoja kupigwa nchini Uingereza kwenye dimba la Stamford Bridge kati ya Chelsea na FC Barcelona.

Mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba akishangilia bao alilofunga wakati wa mchezo wao na FC Barcelona
Mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba akishangilia bao alilofunga wakati wa mchezo wao na FC Barcelona Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mchezo huo ambao FC Barcelona walipewa nafasi kubwa ya kuweza kushinda mchezo huo, mambo yalikuwa tofauti kwani walijikuta wakiangukia pua kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Chelsea.

Barca ambao kwa muda wote wa mchezo walikuwa wanautawala vilivyo walijikuta wakikubali kufungwa katika dakika za nyongeza kabla ya kwenda mapumziko, bao lililofungwa na mshambuliaji Didier Drogba.

kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu ya Barcelona kuzidisha mashambulizi kwenye lango la Chelsea huku washambuliaji wake wakikosa mabao ya wazi kwenye kipindi hicho lakini hawakufua dafu.

Chelsea walianza kucheza mchezo wa kujilinda kwa dakika zote tisini na kufanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 1-0 huku kwenye mchezo wa marudiano juma moja lijalo ukitarajiwa kuwa mgumu kwa timu zote mbili.

Kocha wa Barcelona, Pep Guardiola amekiri timu yake kupoteza nafasi nyingi za wazi lakini akaipongeza Chelsea kwa kulinda goli vizuri kiasi cha kuzuia wachezaji wake kupata nafasi za kufunga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.