Pata taarifa kuu
LIGI YA MABINGWA ULAYA

Leo ni leo nusu fainali ya kwanza ya ligi ya mabingwa Ulaya, Bayern Munich vs Real Madrid

Ligi ya mabingwa barani Ulaya hii leo inatarajiwa tena kuanza kutimua vumbi kwenye kiwanja kimoja pekee, kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza kati ya timu za Bayern Munich ya Ujerumani na Real Madrid ya Uhispania.

Kocha wa Real Madrid Josee Mourinho
Kocha wa Real Madrid Josee Mourinho Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mchezo huo ambao unatarajiwa kupigwa kwenye dimba la Allianz Arena mjini Munich Ujerumani, tayari umevuta hisia za mashabiki wengi wa soka barani Ulaya kulinga na upinzani wa jadi ulizonazo timu hizo zinapokutana kwenye ligi ya mabingwa.

Vijana wa Josee Mourinho tayari wamewasili mjini Munich toka mwishoni mwa juma na wamekuwa wakifanya mazoezi makali kujiwinda na mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa mkali na wakusisimua kwa muda wote wa mchezo.

Madrid inatarajiwa kuwatumia wachezaji wake nguli akiwemo mfungaji wake mahiri Christian Rinaldo, Ricardo Kaka, Karim Benzema na Gonzalo Higuan.

kwa upande wa klabu ya Bayern Munich, kocha mkuu wa timu hiyo Yuppe Heynckes amesema kuwa anafahamu kuwa mchezo wa leo utakuwa mgumu lakini ana imani kuwa wachezaji wake watafanya kila linalowezekana kushinda mchezo wa leo.

Nahodha wa klabu hiyo Philip Lahm amesema kuwa wachezaji wenzake wako kwenye morali ya hali ya juu na kwamba wamepania kushinda mchezo wa leo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.