Pata taarifa kuu
FA CUP

Fainali ya kombe la FA nchini Uingereza ni Liverpool na Chelsea, May 5

Hatimaye timu ambazo zitacheza fainali ya kombe la FA nchini Uingereza zimefahamika kufuatia mchezo wa siku ya jumapili uliowakutanisha timu za Tottenham na Chelsea.

Kocha wa Tottenham Harry Redknap akimlalamikia mwamuzi wa mchezo baada ya kuwazawadia Chelsea goli lenye utata
Kocha wa Tottenham Harry Redknap akimlalamikia mwamuzi wa mchezo baada ya kuwazawadia Chelsea goli lenye utata Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwenye mchezo wa hapo jana, Tottenham wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa White Hart Lane walijikuta wakishindwa kufua dafu mbele ya Chelsea, baada ya kukubali kichapo cha mabo 5-1.

Kwenye mchezo huo ambao Chelsea walionesha toka mwanzo walidhamiria kushinda, walipata bao la lwa kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Didier Droba na baadae Juan Mata kuandika bao la pili kabla ya Tottenham hawajapata bao la kufutia machozi.

Mchezo huo ulishuhudia Chelsea wakizawadiwa goli lenye utata baada ya mlinda mlango wa Tottenham kufanyiwa madhambi na mpira kutokuvuka mstari lakini mwamuzi aliwazawadia goli.

Goli hilo limezua mjadala mkubwa kuhusu kutumika kwa teknolojia ya kuangalia goli kwenye mstari.

Kwa matokeo hayo ni wazi sasa Chelsea itakutana na Liverpool kwenye fainali itakayopigwa tarehe 5 ya mwezi ujao.

Liverpool wamefuzu hatua baada ya kuwafunag Everton kwa mabao 2-1.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.