Pata taarifa kuu
Tenis

Andy Murry kuchuana na Rafael Nadal

Andy Murray mchezaji wa tano kwa ubora duniani kwa upande wa wanaume atachuana na Rafael Nadal anayeorodheshwa wa pili duniani katika nusu fainali ya mashindano ya Miami Masters siku ya Ijumaa.

Rafael Nadal
Rafael Nadal Reuters
Matangazo ya kibiashara

Murray alifanikiwa kufika katika hatua hiyo ya nusu fainali baad aya kumshinda Mserbia Janko Tipsarevic kwa seti za 4-6 ,6-3, 6-4.

Rafael Nadal naye alimshinda Jo Wilfried kutoka Ufaransa kwa seti za
6-2 5-7 6-4 katika robo fainali.

Kwa upande wa akina dada, Marion Bartoli wa Ufaransa anayeorodheshwa wa saba dunaini alimshinda Victoria Azarenka kutoka Belarus anayeorodheshwa wa kwanza dunia kwa seti za 6-3, 6-3.

Azarenka ambaye amekuwa akishinda mataji mbalimbali kuanzia mwaka huu likiwemo Australian Open, Sydney, Doha na mashindano ya India, ambaye amesema baada ya kushindwa kuwa yeye ni binadamu tu wa kawaida na pia wakati mwingine anaweza kushindwa.

Bartoli atacheza na Agnieszka Radwanska wa Poland aliyemshinda Venus William kutoka Marekani.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.