Pata taarifa kuu
ZURICH

Fifa kutoa bima ya afya kwa wachezaji wakati wa mechi za kimataifa

Rais was shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter amesema shirikisho hilo litahakikisha kuwa wachezaji wote wanapata bima ya afya  wakati wanapocheza katika mechi zote za kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Blatter amewaambia wajumbe wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kuwa,vyama vya soka kote duniani vitatia saini makubaliano hayo kufikia mwezi Mei mwaka huu.

Wachezaji watakaonufaika na mpango huo ni wale wote watakaochezea timu zao za taifa na vlabu katika mechi zote zinazotambuliwa na FIFA.

Tayari shirikisho la soka barani Ulaya Uefa, limetangaza kuwa litaanza zoezi la kutoa bima kwa wachezaji wote wakati wa michuano ya bara Ulaya  baadaye mwaka huu.

Mpango wa kupewa bima kwa wachezaji  unakuja wakati, Fabrice Muamba mchezaji wa Bolton Wanderers wa klabu ya soka nchini Uingereza akipata nafuu katika hospitali ya moyo jijini London Uingereza baada ya kuzirai uwanjani mwishoni mwa wiki iliyopita.

Daktari wa klabu hiyo Jonatahan Tobin anasema ni muujiza kuwa Muamba anaimarika lakini alikuwa amekata roho kwa muda wa dakika 78 wakati alipofikishwa hospitalini na juhudi za madakatari ndizo zilizomwokoa.

Kocha wa Bolton Owena Coyle amesema wachezaji wake watapata ugumu kucheza vema dhidi ya Blackburn siku ya Jumamosi kutokana na kulazwa kwa Muamba .
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.