Pata taarifa kuu
ZURICH

Real yatakiwa kutoidharau Apoel

Real Madrid imetakiwa kuwaheshimu wapinzani wao Apoel Nicosia katika michuano ya robo fainali ya ligi ya mabingwa pamoja na klabu hiyo kuwa na historia ya unyenyekevu.

Nahodha wa Real Madrid,Jose Mourinho
Nahodha wa Real Madrid,Jose Mourinho
Matangazo ya kibiashara

Hayo yamesemwa na Meneja wa kikosi hicho Jose Mourinho siku ya jumamosi na kutanabaisha kuwa Apoel wametinga robo fainali kwakuwa wamestahili ingawa haina sifa tukuka ukilinganisha na timu nyingine lakini bado inapaswa kuheshimika.

Meneja huyo aliongeza kuwa kiungo wake mchezaji wa kati Xabi Allonso hatakuwepo kutokana na kusimamishwa lakini nahodha huyo mreno akasema kuwa kutokuwepo kwa mchezaji huyo hakuyumbishi jambo lolote.

Kiongozi huyo amewataja wachezaji ambao wanatarajiwa kusakata kabumbu kwa niaba ya mchezaji kiungo wa kati ambapo Sahin, Lass (Diarra), Granero, ambao wote ni viungo wa kati wanauwezo wa kucheza kwa niaba ya Xabi.

Kiokosi hicho kinatarajia kukipiga na Malaga hapo jumapili huku Mourinho akimwondoa raia wa Uturuki Nuri Sahin, ambaye amewasili Real msimu uliopita na bado hajacheza mechi.

Nahodha huyo pia amepangua shutuma za uzushi kuwa alipangwa kutangaza kuwa Sahin angecheza kwa mkopo msimu ujao na kusema mchezaji huyo ataendelea kuwepo katika msimu ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.