Pata taarifa kuu
UINGEREZA-AUSTRALIA

Jake White akiri mabosi wa RFU kumfuata wakitaka afundishe timu ya taifa ya raga, Uingereza

Kocha wa timu ya mchezo wa raga ya Brumbies ya nchini Australia ambaye pia waliwahi kutwaa ubingwa wa dunia akiwa na timu ya taifa ya Afrika Kusini mwaka 2007 Jake White amekiri kufuatwa na mabosi wa Uingereza. 

Kocha wa timu ya mchezo wa Raga ya Brumbies ya Australia ambaye anawaniwa na chama cha Uingereza kukinoa kikosi cha timu ya taifa
Kocha wa timu ya mchezo wa Raga ya Brumbies ya Australia ambaye anawaniwa na chama cha Uingereza kukinoa kikosi cha timu ya taifa Reuters
Matangazo ya kibiashara

White ambaye mara kadhaa ametajwa kuwa mrithi wa kocha wa timu ya taifa ya Uingereza baada ya kocha wake martin Johnson kubwaga manyanga amekuwa akiwindwa na chama cha mchezo huo cha nchini Uingereza RFU.

Akihojiwa na kituo kimoja cha redio White amekiri kufuatwa na mabosi wa Uingereza kumtaka akinoe kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza na kuongeza kuwa yupo tayari lakini mpaka pale atakapo maliza michuano ya Super 15 na timu yake ya sasa.

RFU imekuwa katika mchakato wa kumsaka kocha mkuu wa timu hiyo ambapo mwishoni mwa juma hili inatarajiwa kumafnyia mahojiano kocha wa muda Stuart Lancaster ambaye akuwa na timu hiyo kwa muda sasa.

Endapo white atashikilia msimamo wake basi Uingereza itamaliza mashindano ya Six nations ikiwa na kocha wa muda pamoja na kuelekea nchini Afrika Kusini kwa mechi ya kimataifa dhidi ya timu hiyo.

Uingereza inatarajiwa kushuka uwanjani Jumapili hili kukabiliana na Ufaransa kwenye mashindano ya Six Nations kabla ya kumaliza kutetea ubingwa wake na timu ya Jamhuri ya Ireland tarehe kumi na saba ya mwezi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.