Pata taarifa kuu
LIGI YA MABINGWA ULAYA

Licha ya kutupwa nje klabu ya Arsenal yaifanyia mauaji AC Milan

Licha ya kupoteza mchezo wa awali na kuwa na matumaini finyu ya kuweza kufuzu kwenye hatua inayofuata klabu ya Arsena jana ilifanya kweli na kufanikiwa kuwasambaratisha AC Milan kwa magoli 3-0.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger akilalama kwa mwamuzi wakati wa mechi ya timu yake na AC Milan hapo jana
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger akilalama kwa mwamuzi wakati wa mechi ya timu yake na AC Milan hapo jana Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa kwenye uwanja wake wa Nyumbani wa Emirates klabu ya Arsenal iliwapa raha mashabiki wake baada ya kufanikiwa kumaliza mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya AC Milan kwa mabao matatu kwa bila.

Kwenye mchezo huo ambao klabu ya Arsenal iliuanza kwa kasi toka dakika za mwanzo iliwachukua dakika saba tu kuandika bao kupitia kwa Laurent Koscielny aliyetumia vema makosa ya mabeki wa AC MIlan.

Katika dakika ya ishirini na sita Arsena walifanikiwa kupata bao jingine kupitia kwa Tomas Rosicky kabla ya dakika ya 44 Robin Van Parse hajaiandikia bao la tatu klabu yake.

Mpaka mpira unamalizika Arsenal walifanikiwa kuongoza kwa mabao matatu kwa bila lakini walishindwa kufuzu hatua inayofuata baada ya kutofautiana magoli ya kufungwa huku mechi ya awali Arsenal wakifungwa mabao manne.

Mchezo mwingine uliwakutanisha klabu ya Benfica ambayo ilikuwa na kibarua dhidi ya klabu ya Zenit Petersburg na kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabo mawili kwa bila na hivyo kufuzu kwenye hatua ya robo fainali ya michuani hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.