Pata taarifa kuu
LIGI YA MABINGWA ULAYA

Kitimtim kingine cha klabu bingwa ulaya leo

Ligi ya mabingwa barani Ulaya inatarajiwa kuendelea tena hii leo kwa miamba kadhaa ya soka kushuka viwanjanai kupepetana kutafuta nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali.

Wachezaji wa FC Barcelona wakiwa kwenye mazoezi kabla ya mechi ya leo
Wachezaji wa FC Barcelona wakiwa kwenye mazoezi kabla ya mechi ya leo Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hii leo kwenye michuano hiyo klabu nne zinatarajiwa kushuka viwanjanai kupepetana kutafuta nani mbabe wa kuweza kufuzu kwenye hatua inayofuata michezo ambayo inatarajiwa kuwa ya kuvutia sana.

Mchezo wa awali utawakutanisha timu ya APOEL Nicosia ambayo itakuwa na kibarua dhidi ya timu ya Lyon ya nchini Ufaransa kwenye mchezo ambao unatazamwa na watu wengi kufutia mchezo wao wa awali kuwa wa upinzani mkubwa.

Makocha wa pande zote mbili wamejigamba kila mmoja wao kuibuka na ushindi huku huku wakisisitiza kuwa mwamuzi wa mwisho ni refarii na dakika tisini ambazo watakuwa wanatifuana.

Mchezo mwingine unatarajiwa kuwakutanisha mabingwa wa Dunia na mabingwa wa kombe hilo klabu ya FC Barcelona ambao watakuwa nyumbani kwenye dimba la Nou Camp kuwakaribisha ndugu zao FC Beyern Liverkusen kwenye mchezo ambao pia utakuwa wa oatashika nguo kuchanika.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.