Pata taarifa kuu
UEFA

Arsenal kwenye mtihani mwingine wa klabu bingwa barani ulaya dhidi ya AC Milan

Ligi ya mabingwa barani Ulaya inatarajiwa kutimu vumbi tena hii leo ambapo miamba kadhaa itashuka viwanjani kuonyeshana ubabe katika hatua ya mtoano kufuzu robo fainali. 

Mchezaji wa Arsenal Theo Walcot akikabiliana na mchezaji wa AC Milan wakati timu hizo zilipokutana majuma kadhaa yaliyopita
Mchezaji wa Arsenal Theo Walcot akikabiliana na mchezaji wa AC Milan wakati timu hizo zilipokutana majuma kadhaa yaliyopita Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mchezo ambao unavuta hisia za watu wengi ni ule ambao utawakutanisha klabu ya washika bunduki wa London Arsenal ambao watawakaribisha AC Milan ya Italia kwenye mchezo ambao Arsenal ni lazima ishinde kwa mabao manne ili kuweza kusonga mbele.

Kwenye mchezo wa awali Arsenal ilikubali kulala ugenini kwa mabao manne kwa nunge kwenye mchezo ambao vijana wa kocha Arsene Wenger walishindwa kabisa kuhili kwata la wachezaji wa AC Milan ambao toka awali walionyesha dhamira ya kuibuka na ushindi.

Akizungumzia mchezo wa hii leo, kocha Arsene Wenger amekiri kuwa mchezo utakuwa mgumu lakini lolote linaweza kutokea uwanjani ikiwemo matokeo kubalika na wao kuchomoza na ushindi wa kishindo na hatimaye kufuzu.

Mechi nyingine ni ile ambayo itawakutanisha timu ya Benfica ya Uturuki ambayo itakuwa na kibarua dhidi ya klabu ya Zenit Petersburg mchezo ambao nao pia unapewa nafasi kubwa kwa timu zote mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.