Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Kocha wa Chelsea Villas-Boas akiri mustakabali wake upo mashakani Stamford Bridge

Kocha Mkuu wa Klabu ya Chelsea Andre Villas-Boas amekiri hadharani anahofu huenda tajiri wa timu hiyo Mrusi Roman Abramovich akamtimua iwapo atashindwa kupata mafanikio ambayo yamekuwa ndoto huko Stamford Bridge.

Kocha wa Chelsea Andre Villas-Boas akiwa na mchambuliaji wake Didier Drogba kabla ya mchezo wao na Napoli wa Ligi ya Mabingwa nchini Italia
Kocha wa Chelsea Andre Villas-Boas akiwa na mchambuliaji wake Didier Drogba kabla ya mchezo wao na Napoli wa Ligi ya Mabingwa nchini Italia REUTERS/Tony Gentile
Matangazo ya kibiashara

Villas-Boas mwenye umri wa miaka 34 rais wa Ureno ameonesha hofu yake kwa mara ya kwanza ba kuweka bayana kuna kila dalili za yeye kufuata nyendo za Carlo Ancelotti ambaye alifungashiwa virago baada ya kuwa na msimu mbaya.

Villas-Boas ambaye amekuwa akipata uungwaji mkono wa hali ya juu kutoka kwa Abramovich amekuwa na matokeo mabaya katika siku za hivi karibuni na kujikuta akiwa amesalia kwenye hatua ya Mtoano ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya huku kwenye Ligi akiendelea kuchechemea.

Kocha huyo aliyejiunga na Chelsea akitokea FC Port ya Ureno amesema hofu ya yeye kuondoka imeongezeka kutokana na tabia ya Abramovich ya kutimua makocha licha ya mwanzoni kuonesha kuwaunga mkono.

Kocha huyo kijana amesema haelewi kile ambacho kinaweza kutokea kesho au hata baada ya miaka miwili iwapo ataendelea kukikoa kikosi cha The Blues ambacho kwa sasa kinashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza.

Chelsea ipo pointi kumi na saba nyuma wa vinara wa Ligi Kuu nchini Uingereza Manchester City huku pia wakiwa na kibarua kwenye Ligi ya Mabingwa kutokana na kupata kichapo cha mbwa mwizi kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Napoli cha magoli 3-1.

Katika hatua nyingine Villas-Boas ameanza harakati zake za kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao baada ya kuonesha nia ya kutaka ya kumsajili mshambuliaji wa Porto Hulk ambaye ndiyo nguzo ya ushambuliaji kwa Klabu hiyo.

Villas-Boas amesema ameamua kuchukua hatua hiyo kutokana na baadhi ya wachezaji umri wao kwenda huku Salomon Kalou na Florent Mlouda wakielekea kumaliza mikataba yao waliyonayo.

Kocha huyo hakushindwa kuanisha wachezaji ambao anaona kama nguzo ya baadaye ya timu hiyo akiwemo Juan mata ambaye amesajiliwa msimu huu akitokea Valencia na kinda wa Kiingereza Daniel Sturridge.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.