Pata taarifa kuu
UHISPANIA

Real Madrid yaichelewesha Barcelona kutwaa Ubingwa wa Ligi

Magoli matatu ya Kiungo Mshambuliaji wa Kimataifa wa Ureno anayesukuma ngozi katika Klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo yameifanya timu ya Barcelona kuchelewa kutangazwa mabingwa na hivyo wanalazimika kupata pointi moja ili wawe mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo.

Kiungo Mshambuliaji wa Klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo akishangilia moja ya magoli yake kwenye Ligi Kuu nchini Uhispani LA LIGA
Kiungo Mshambuliaji wa Klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo akishangilia moja ya magoli yake kwenye Ligi Kuu nchini Uhispani LA LIGA REUTERS/Susana Vera
Matangazo ya kibiashara

Mesut Ozil Kiungo wa pembeni wa Kimataifa wa Ujerumani ndiye ambaye alifunga goli la kwanza la Real Madrid kwenye ushindi huo mnono wa magoli 4-0 mbele ya Getafe kabla ya Ronaldo hajaanza balaa la kufunga magoli mengine.

Reald Madrid wakiwa katika dimba lao la nyumbani la Santiago Bernabeu walikuwa wanacheza kwa uhakika na kuwachanganya wapinzani wao ambao walikubali kichapo kwa urais.

Baada ya kukamilika kwa mpambano huo wa Real Madrid hii leo Mabingwa watetezi wa LA LIGA Barcelona itakuwa na kibarua cha kutangaza ubingwa mapema mbele ya Levante iwapo itapata pointi moja.

Kama Real Madrid ingefungwa katika mchezo wao wa jana ingetoa nafasi kwa Barcelona kutwaa ubingwa kabla hata ya mchezo wao wa leo lakini sasa wanahitajika kupata sare tu ili watwae Kombe la Ligi Kuu Nchini Uhispani LA LIGA.

Kwa mwenendo wa LA LIGA ulivyo hivi sasa ni wazi Real Madrid hawana nafasi ya kutwaa Kombe msimu huu lakini Ronaldo anasaka kwa udi na uvumba tuzo ya ufungaji bora kwa mwaka.

Ronaldo mwenye magoli 36 kwa sasa amemuacha mpinzani wake Lionel Messi kwa tofauti ya magoli 5 anasaka kuweka rekodi ya kufunga magoli mengi kwenye LA LIGA ambayo iliwekwa na Hugo Sanchez na Telmo Zarra ambao kila mmoja alishawahi kufunga magoli 38.

Barcelona kwa upande wao wanasaka kuweka rekodi ya kuwa Klabu ya kwanza katika kipindi cha karibuni kufanikiwa kutwaa Ubingwa wa LA LIGA kwa misimu mitatu mfululizo.

Kikosi hicho cha Kocha Pep Guardiola kinataka kushinda Ubingwa wa nyumbani mapema ili waanze maandalizi ya Mchezo wao wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya UEFA dhidi ya Manchester United utakaopigwa kwenye Uwanja wa Wembley tarehe 28 ya mwezi May.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.