Pata taarifa kuu

Kupitishwa kwa chanjo: Jean Castex ataka ‘mjadala haraka iwezekanavyo’

Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex amekuwa bungeni Jumatano hii, Januari 5, baada ya mkutano uliogubikwa na maswali mengi siku moja kabla, kufuatia matamshi ya kutatanisha ya rais wa Jamhuri juu ya "nia" yake "kukabaliana" na wale ambao hawakuchanjwa.

Waziri Mkuu Jean Castex akizungumza mbele ya Bunge la taifa mjini Paris, Jumatano hii, Januari 5, 2022.
Waziri Mkuu Jean Castex akizungumza mbele ya Bunge la taifa mjini Paris, Jumatano hii, Januari 5, 2022. AFP - BERTRAND GUAY
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Ufaransa alitoa wito kwa wabunge "kujadiliana haraka iwezekanavyo" kuhusumuswada wa kuanzishwa kwa hati ya chanjo, uchunguzi ambao ulikuwa umesitishwa Jumanne jioni katika hali tete.

"Ni jukumu lenu kujadili haraka, kwa kuzingatia hali ya nchi yetu, ya Ulaya", amesema Bw. Castex Jumatano hii mbele ya Bunge, siku moja baada ya kikao chenye kilichokubikwa na maswali mengi.

Waziri Mkuu alirejelea kauli ya Emmanuel Macron kuhusu wale ambao hawajachanjwa kwa masharti haya: “Kuna ugumu wa wananchi wenzetu wanaokataa kuchanjwa. Hapa sijamtukana mtu, ni ukweli. "

"Kuwa huru haimaanishi kuwaambukiza wengine bila kuadhibiwa, si kusumbua idara zetu za afya ambazo tayari zinakabiliwa na mambo mengi," amebaini Jean Castex, akitaka "jukumu la kibinafsi la kila raia wa Jamhuri."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.