Pata taarifa kuu

Israel yatangaza kumrejesha nyumbani balozi wake katika Umoja wa Mataifa

Israel imetangaza siku ya Jumatatu kumrejesha nyumbani balozi wake katika Umoja wa Mataifa kwa mashauriano, ikishutumu Umoja wa Mataifa kwa kupendelea Hamas kabla tu ya kuchapishwa kwa ripoti ya unyanyasaji wa kingono uliofanywa na kundi la Wanamgamo wa Kipalestina la Hamas mnamo Oktoba 7.

Wanadiplomasia wa Israel wamekuwa wakiongeza vitendo vyao vya kushangaza na mashambulizi ya wazi dhidi ya Umoja wa Mataifa na maafisa wake kwa wiki kadhaa. Hapa, Balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa Gilad Erdan akizungumza akiwa amevalia nyota ya njano, wakati wa mkesha mjini New York mnamo Novemba 6, 2023.
Wanadiplomasia wa Israel wamekuwa wakiongeza vitendo vyao vya kushangaza na mashambulizi ya wazi dhidi ya Umoja wa Mataifa na maafisa wake kwa wiki kadhaa. Hapa, Balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa Gilad Erdan akizungumza akiwa amevalia nyota ya njano, wakati wa mkesha mjini New York mnamo Novemba 6, 2023. © Peter K. Afriyie / AP
Matangazo ya kibiashara

"Nimemuagiza balozi wetu katika Umoja wa Mataifa, Gilad Erdan, kurejea Israel kwa ajili ya mashauriano ya haraka kufuatia jaribio la kunyamazisha ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu ubakaji mkubwa uliofanywa na Hamas na washirika wake mnamo Oktoba 7," Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Katz amesema katika ujumbe uliochapishwa kwenye X.

Mateka 130 bado wanashikiliwa huko Gaza kulingana na Israeli

"Ni wakati wa kuchukua hatua," amesema katika ujumbe mwingine, akihutubia Antonio Guterres. "Hamas lazima itambuliwe kimataifa kama kundi la kigaidi" na "kujiondoa kwa UNRWA kutoka Gaza ni muhimu," ameongeza.

Kulingana na Israel, mateka 130 bado wanazuiliwa huko Gaza, 31 kati yao wanaaminika kufariki, kati ya karibu watu 250 waliotekwa nyara Oktoba 7.

Operesheni za kijeshi zilizoanzishwa kwa kulipiza kisasi na Israel zimesababisha vifo vya takriban watu 30,534, wengi wao wakiwa raia, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Hamas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.