Pata taarifa kuu

Joe Biden atangaza kuwepo na maendeleo katika usitishwaji mapigano Gaza

Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza siku ya Jumamosi, Novemba 4, kuwepo kwa maendeleo katika "usitishwaji wa mapigano kwa minajili ya kutoa misaada ya kibinadamu" lililotakiwa na Washington katika mapigano kati ya Israel na Hamas huko Gaza, utakaowezesha kusaidia kulinda raia na kusafirisha vifaa zaidi.

Wapalestina wakikagua vifusi vya nyumba iliyoharibiwa na mashambulizi ya Israel huko Gaza, Novemba 4, 2023.
Wapalestina wakikagua vifusi vya nyumba iliyoharibiwa na mashambulizi ya Israel huko Gaza, Novemba 4, 2023. AP - Abed Khaled
Matangazo ya kibiashara

Alipoulizwa kama kuna maendeleo katika suala hili, Joe Biden amejibu "ndiyo", alipokuwa akitoka kanisani huko Delaware, kabla ya kuingia kwenye gari lake, hata kama mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya eneo la Wapalestina linalodhibitiwa na Hamas yakiendelea.

Akiondoka katika Kanisa la Kirumi la St. Edmond katika Ufuo wa Rehoboth, Delaware mnamo Novemba 4, 2023, rais wa Marekani alijibu kwa uthabiti kuhusu maendeleo ya kupata utulivu wa kibinadamu huko Gaza, eneo linaendelea kushambuliwa na Israeli.

Wakati huo huo Maandamano ya familia na wafuasi wa mateka wanaoshikiliwa na Hamas yaliwaleta pamoja maelfu kadhaa ya watu huko Tel Aviv Jumamosi jioni, wakidai juhudi zaidi kutoka kwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ili kuwakomboa. Huko Jerusalem pia, mamia ya watu pia wameandamana kumtaka Benjamin Netanyahu ajiuzulu, ambaye alichukuliwa kuwa "anawajibika na ana hatia" kwa kushindwa katika usimamizi wa nchi. Miongoni mwa waandamanaji, baadhi pia wametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano huko Gaza.

Mashambulizi ya Oktoba 7 yaliyotekelezwa na Hamas yalisababisha vifo vya takriban watu 1,400 nchini Israel. Pia kuna angalau watu 240 wameshikiliwa mateka.

Wkati huo huo jeshi la Israel limeendelea na mashambulizi yake ya ardhini katika Ukanda wa Gaza Jumamosi, Novemba 4. Siku ya Ijumaa lilitangaza kwamba limeuzingira mji wa Gaza baada ya wiki kadhaa za mapigano ya ardhini na mashambulizi mabaya katika ardhi ya Palestina. Wiki nne baada ya kuanza kwa mzozo huo, idadi ya vifo imezidi watu 10,000. Wito wa "kusitishwa kwa mapigano" na maandamano ya kupinga vita yanaongezeka duniani kote. Serikali ya Israel inasisitiza kwamba "itampata na kumuangamiza" afisa wa kundi la Hamas Yahya Sinouar huko Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.